• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 1202

    (GMT+08:00) 2013-12-05 16:53:33
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Geofrey Wandera Namachi wa Eveready Security Guard wa S.L.P 57333 Nairobi Kenya, anaanza kwa kusema kutokana na kuanzisshwa kwa utaratibu mpya wa kurusha matangazo, idhaa ya Kiswahili ya redio China Kimataifa CRI imepata mafanikio bora yenye ufanisi wa hali ya juu, kwani mabadiliko ambayo CRI inayashuhudia kwa sasa ni miongoni mwa hatua mahsusi ambayo CRI imeyapata. Kwa sasa CRI inasikika na kuvuma bila ya matatizo yoyote.

    Pamoja na hayo CRI imepata watangazaji wenye tajriba kubwa katika nyanja hii ya utangazaji, isitoshe vipindi ambavyo vimeanzishwa hivi karibuni ni vipindi ambavyo watu wengi hivi sasa wanavifuatilia kwa karibu sana. Kwahakika kila kipindi kinaniridhisha sawasawa, kwani uchambuzi na maelekezo ni mzuri kabisa. Kwasasa CRI imejitolea muhanga na inaridhisha kwa kila namna, iwe burudani ni chungu nzima, uchambuzi wa uchumi na biashara si haba.

    Maswala ya michezo CRI pia imepiga hatua kabambe kuelimisha wasikilizaji wake yanayojiri kote viwanjani. Pamoja na hayo kipindi cha safari ya mwandishi ni miongoni mwa vipindi vinavyopendwa zaidi. Mwisho nawapa hongera kwa kufanikisha matangazo ya CRI kusikika Zanzibar katika masafa ya 99.7FM ambapo Nairobi inasikika katika masafa ya 91.9FM. kweli CRI inakuwa kwa kasi mno. Nisingependa kusahau kuwafahamisha kuwa barua zote mnazonitumia huwa nazipokea kwa njia nzuri sana. Ishara kuwa posta za Kenya na China zina ushirikiano mzuri wa haki na kweli. Naomba ushirikiano na urafiki wangu na CRI udumu milele.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Geofrey Wandera Namachi kwa barua yako, kwa kweli tunasema ahsante sana kwa pongezi ulizotoa kuhusu matangazo na vipindi vyetu, kwani idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa inajitahidi kadiri iwezevyo kuwaridhisha wasikilizaji wake, tunatumai kuwa sio wewe tu uliyeridhika bali wasikilizaji wetu wote. Ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Gulam Haji Karim wa S.L.P 504 Tanzania anasema salamu nyingi kutoka Lindi, baada ya salamu napenda kujua hali zenu natumai mu wazima wa afya, kwa upande wangu mambo ni mazuri kabisa. Naomba nipatiwe ushauri wa namna ya usikilizaji mzuri wa matangazo kwani bado nipo kizani hapa mkoa wa kusini, kwani mji huu upo chini sana kutoka usawa wa bahari.

    Najaribu sana kufuatilia matangazo ya CRI saa 1 inaanza taarifa ya habari muda si mrefu mawasiliano yanachafuka na hapo sijui hii inatokana na nini, najaribu kufunga antenna waya wa shaba ili kuvuta matangazo lakini wapi, naondokea patupu. Labda nisubiri mitambo ya FM kama Zanzibar nakutakieni kazi njema.

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Gulam Haji Karim kwa barua yako fupi ambayo tumechelewa kuipata, pia tunapenda kukupa pole kwa usumbufu unaopata, lakini jambo la kufurahisha ni kwamba hivi sasa tumeshaanzisha matangazo yetu kule Zanzibar, ila wasiwasi wetu ni kwamba hatujui kama unatupata au bado unakabiliwa na matatizo ya usikivu, pole sana.

    Mwisho tunawaletea barua tulizotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Wilfred Thuita anasema ni mimi shabiki wenu wa dhati nasema hivi nimefurahia sana vipindi vyenu kutoka Radio China Kimataifa.

    Naye Adad anasema naomba tu nchi ya China iendelee kuwekeza Afrika

    Frank Mmassy Odiero wa SL.P 860 Zanzibar Malindi anasema CRI mnatisha kwani ninyi ni wapekee Afrika Mashariki kwa sisi wapenzi kupata faida nyingi kutoka kwenu kama habari, kujua Kichina, masuala ya kiuchumi, na mwisho nawakumbuka Kadogoo, Wayuha, Kaswitii wakiwa Kenya, Peter Mmassy na Oscer Mwacha wakiwa Mwanza Tanzania, mnatisha tutaendelea wasapoti vilivyo, xiexie.

    Na mwisho ni msikilizaji wetu Maridadi Wilbert baruapepe yake ni r.maridadi@gmail.com anasema nawapa kongole jamani hakika mnatutoa kimasomaso wachina sisi kwetu huku hatupendi vya kwetu.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote mliotutumia maoni na mapendekezo yenu kwenye mtandao wetu tunawaomba muendelee kusikiliza matangazo na vipindi vyetu na kutoa maoni zaidi ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako