• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 1231

    (GMT+08:00) 2013-12-31 16:36:58
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Mwalimu Maurice Nawate Okumu wa S.L.P 798 Mumias Kenya anasema nachukua fursa hii kuipongeza CRI, wakurugenzi na watangazaji wote kwa kazi nzuri wanayofanya kupitia redio hii, kwanza wanaendeleza matumizi ya lugha yetu ya mashariki mwa Afrika. Pili kupitia lugha yetu hii kunapatikana nafasi za kujifunza kichina lugha ambayo inatumiwa na robo nzima ya watu ulimwenguni. Na mwisho tunapata kujulishwa matukio mbalimbali ulimwenguni na hata kujifunza utamaduni wa wachina, ombi langu tu ningeomba kujiunga na wanachama wa salamu kupitia CRI. Ahsante sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Mwalimu Maurice Nawate Okumu kwa barua yako fupi, pia tunapokea kwa mikono miwili pongezi ulizotoa kwa wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa, kama ulivyosema kweli tunajitahidi kueneza Kiswahili kwani tunajua ni lugha inayoongewa sana si Afrika Mashariki tu bali hata sehemu nyingine za Afrika, ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya barua ya Bwana Wambura Mwita Nyamhanga wa S.L.P 158 Tarime Mara Tanzania anasema nilifurahi sana hasa pale niliposoma vijarida vya CRI sambamba na kusikiliza redio na kupata habari kwamba redio China kimataifa imetimiza miaka 70 tangu ianzishwe. Hivyo hizi ni pongezi kwa redio hii ambayo haina kinyongo redio nyingine, Club au sekta zozote zile za urushaji habari duniani. Hata hivyo kutokana na CRI kuwa makini na imara katika uwajibikaji wake, imekuwa ikijiongezea umaarufu wake siku hadi siku hapa barani Afrika na kwingineko duniani.

    Nilifurahi sana kuona kwamba CRI inavilabu zaidi ya 1000 ambapo pia ni redio pekee ambayo hutangaza kwa lugha nyingi zaidi kuliko nyingine duniani.

    Hata hivyo ukweli kwamba CRI haina ubaguzi wowote kwani hata hupokea watangazaji kutoka pembe mbalimbali za dunia bila kujali kabila, taifa au bara walikotokea. Kutokana na hayo yote ni kuonesha ni jinsi gain inavyojali na kulinda maslahi ya haki za binadamu katika pande zote ulimwenguni. Ni imani yangu kwamba redio hii itazidi kuboreka siku hadi siku kutokana na wafanyakazi wake jinsi walivyo wachangamfu, wakakamavu na wenye uzoefu uliobobea katika nyanja hii ya utangazaji.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Wambura Mwita Nyamhanga kwa barua yako, ni kweli CRI imetimiza miaka 70 mwaka jana na kulikuwa na sherehe kubwa ya kupongeza kufikisha miaka yote hiyo. Hivi sasa CRI inaendelea kujikusanyia mashabiki kutoka pande mbalimbali za dunia, ahsante sana.

    Barua ya mwisho inatoka kwa msikilizaji wetu Mchi Marco Budeba Shilugala ambaye anatunziwa barua zake na Stephen Magoye wa S.L.P Kahama Shinyanga Tanzania anasema kwanza kabisa natoa shukrani zangu za dhati kwenu ndugu zangu wa China, kwa uhusiano uliopo kati yetu Tanzania na China. Mmetusaidia mambo mengi sana ambayo yametufanya tujenge udugu wa ndani ambao hautavunjika milele. Mimi napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru na kmuwapongeza kupitia kipindi cha sanduku la barua cha idhaa ya kiswahili ya redio China kimataifa.

    Mchango wenu mnaoutoa hatutasahau daima. Hivyo napenda kuwaombea ndugu wa China Mungu azidi kulibariki taifa hili ili liwe na mafanikio zaidi kiuchumi. Mwisho kabisa nawashukuru kwa salamu zenu mlizotoa hewani, nami nilizipokea nikafurahi sana, hata mimi nawasalimu sana ndugu zangu na ningependa mpokee salamu zangu na pia napenda tuungane kupitia idhaa hii kwa kupeana salamu na Mungu akipenda ningependa kufika huko China nijionee mwenyewe taifa hilo lenye maendeleo makubwa kiuchumi.

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Mchi Marco Budeba Shilugala kwa barua yako, tumefurahishwa sana na maoni yako hasa kuhusu uhusiano wetu yaani kati ya Tanzania na China, kama ulivyosema nchi hizi mbili ni marafiki wakubwa ndio maana China haioni muhali kuisaidia Tanzania, nasi tunaziombea nchi hizi mbili ziendelee kushirikiana na kupata mafanikio kwa pamoja pia urafiki huu udumu milele, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako