• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hisia tofauti kuhusu ulipaji wa mahari

    (GMT+08:00) 2014-01-27 10:44:44

    Nchini Kenya kiongozi wa kanisa la Katoliki Kadinali John Njue, anatoa wito kwa wazazi kulegeza kamba katika ulipaji mahari kabla ya harusi kufanyika, ili kusaidia vijana wengi kuoa.

    Lakini hoja hiyo imeanza kuzua hisia tofauti miongoni mwa wakenya, haswa ikizingatiwa kwamba mila na desturi za kiafrika katika maswala ya ndoa, zinahusu utoaji wa mahari kwanza kabla ya msichana kuolewa.

    "Hata ukipewa mahari ya elfu kumi chukua, halafu mahari hiyo nyingine utapewa tu pole pole, kwa sababu ulipaji wa mahari uwezi kuisha."

    Hayo ni matamshi ya Kadinali John Njue akiongea mwishoni mwa juma alipokuwa akiendesha sherehe ya kuwafunganisha pingu za maisha, maharusi katika eneo la Nyeri mkoa wa kati humu nchini.

    Kadinali Njue katika sherehe hizo za harusi alisema kwamba ulipaji wa mahari, na ya lazima ndilo jambo ambalo limefanya vijana wengi humu nchini kukaa bila kuoa, na ikiwa wanapata fursa ya kuoa huwa wanawatorosha wasichana wa wenyewe, bila hata kuwajulisha wazazi wa msichana.

    Baadhi ya wakenya waliozungumza na Radio China Kimataifa wanasema kwamba, ulipaji wa mahari ni jambo la lazima kwa sababu hutoa hakikisho, la kulindwa kwa msichana wao baada ya kuolewa.

    Kulingana na Ben Muhanji ambaye ni mazazi wa wasichana wawili anasema kwamba, kulingana na mila za kiafrika lazima mahari ilipwe, kwanza kabla ya harusi ama msichana kupeanwa katika ndoa.

    Ben anasema kwamba kukaa na msichana bila kulipa mahari, shida huingia iwapo kitu kama kifo kitawajia.

    "Kutoa mahari barani Afrika ni jambo la lazima, kwanza hio mila lazima ifuatye vilivyo.Mahari lazima itolewe hata kama ni ng'ombe mbili.

    Kulingana na mimi ni kwamba ukitaka kujua ni hatari kukaa na mtoto wa watu bila kulipa mahari ni kwamba shida huingia wakati wa kifo.

    Huwa ni lazima mtu akifa azikwe kwake kwa hivyo katika wakati mgumu kama huo unaweza kuletewa shida na jamii ya msichana."

    Matamshi ya Kadinali Njue yamekuja miezi kadha baada ya mswada kufikishwa mbungeni mapema mwaka huu, ukipendekeza mahari kuwa jambo la hiari, kwa kijana anayeoa.

    Lakini tofauti na Muhanji kuhusu ulipaji wa mahari kabla ya msichana kuolewa, Atieno Obura ambaye pia ni mama mzazi wa wasichana watatu, anasema kwake swala la utoaji wa mahari kabla ya msichana kuolewa halifai kutiliwa mkazo na wazazi.

    Kulingana na yeye ni kwamba jambo la muhimu, ni upendo katika ndoa.

    Anasema kwamba wazazi wanafaa kuanza kukubali mahari hata ikiwa kidogo, na kungojea mali iendelee kulipwa kwa hatua.

    "Mahari sio upendo na mahari kulipwa sio lazima, watu wanaweza kuoana bila ya kutoa mahari na waishi vizuri sana, kwa sababu sio kila mtu anaweza kupata hio mahari. Jambo la maana ni ikiwa unajua umeoa motto wa wenyewe na unaweza kutoa mahari kidogo pia unaweza kutoa.

    Lakini shida hutokea kwa wazazi ambao uwa wanaitisha mahari nyingi labda nyumba kubwa ya ghorofa na ng'ombe mia moja.Kwa hivyo ninasema kilea cha maana mno ni heshima kwa wazazi wa msichana na msichana pia na upendo katika ndoa."

    Ali Juma ni kijana wa miaka 26 na anasema yeye anafikiria wanawake waliokuwa wazuri, wa kunyenyekea wamekwisha na sasa wazazi wanafaa kuacha binti zao waolewe bila mahari, kwa sababu ndoa sasa imekuwa ni taabu tupu.

    Juma anaeleza kwamba sasa yeye hawezi lipa mahari, sababu ikiwa ni kuharibika kwa mienendo liyokuwa mizuri wakati wa wazazi wetu.

    "Wasichana wazuri wa kutolea mahari siku hizi hakuna, sababu, wengi sana wameharibika siku hizi ni ngumu sana kupata msichana unayeweza kusema unaweza lipia mahari."

    Katika jamii nyingi za kiafrika kabla ya msichana kuolewa jambo la ulipaji mahari huwa na umuhimu mkubwa, lakini sasa hoja za kutupilia mila hiyo mbali zimeanza kujitokeza.

    Kwa wengi ambao hushindwa na kutoa mahari kabla ya kuoa msichana huwa wanachukuana na kuishi bila sherehe rasmi ya kuoana, aina ya ndoa mabayo Ben Muhanji anapinga.

    Muhanji anasema kama itabidi ndoa kama hio ifanyike, wazazi wa pande zote mbili wanafaa kujua linaloendelea, lakini pia anaona likiwa jambo la hatari, kulingana na mila ya kikwao.

    "Unajua hii aina ya ndoa ya kuja tujaribu maisha ipo lakini inastahili wazazi wa wanandoa wote wawili wajue.Lakini hizi ndoa za mjini hapa Nairobi ni mbaya sana. Kama vile nilipokwambia awali changamoto uja wakati wa kifo."

    Atieno Obura anasema katika wakati wa sasa, wazazi wengi wameanza tabia ya kuitisha mahari nyingi, na kusahahu kwamba katika nyakati za awali mahari ilikuwa mbuzi wachache tu, na pia ng'ombe wasiowengi.

    Anazidi kusisitiza kwamba familia mbili zinazokuja pamoja zinafaa kuuunda urafiki badala ya uadui kwa kuitisha mahari iliyo nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako