• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jinsi gani wachina wanavyojitahidi kulinda faida ya wateja

    (GMT+08:00) 2014-03-14 09:27:34
    Katika nchi nyingi za Afrika kumekuwa na malalamiko kuhusu bidhaa za China, kuna wale wanaosema kuna bidhaa nyingi feki kutoka China, baadhi ya watu wamekuwa hata wakilalamikia baadhi ya huduma zinazotolewa na makampuni ya China kuwa ni hafifu, kwa kuwa wahusika wanaangalia faida zaidi kuliko ubora wa huduma. Leo basi tunaangalia ni jinsi gani wachina wanavyojitahidi kukabiliana na tatizo hii.

    Pili: Wikiendi hii itakuwa ni siku ya haki za mteja, siku hii inaadhimishwa ili kuhakikisha kuwa wateja wa bidhaa mbalimbali wanalindwa kutokana na vitendo vya wafanya biashara wajanja na wadanganyifu. Hali hii ya wafanya biashara kujaribu kufanya ujanja iko kila karibu kila mahali duniani, kwa hiyo siku hii inaadhimishwa ili wateja kukumbushwa haki zao na wafanya biashara kukumbushwa wajibu wao.

    Fadhili: Kwa bahati mbaya sana katika baadhi ya nchi za Afrika ukitaja bidhaa za China unaweza kusikia watu walikalamikia sifa mbaya ya bidhaa, na wengine wanasema feki. Lakini ajabu ni kuwa hizo bidhaa ambazo zinatajwa kuwa feki hapa China hazipatikani, na kama zikipatikana basi ni za kutafuta sana. Baadhi ya watu wanaokuja kutoka nchi za Afrika huwa wanauliza, inakuwaje tukija hapa China zinakotoka hizi bidhaa feki hatuzipati? Lakini tukiwa Tanzania, Kenya au sehemu nyingine za Afrika kuna bidhaa kama hizi? Pili mimi na wewe tumeishi hapa China kwa muda mrefu kwa hiyo ni vizuri tukiwafahamisha wasikilizaji ni vipi wateja wa hapa wanalindwa dhidi ya bidhaa feki.

    Pili: Kwanza sababu kubwa ni kuwa wenzetu wanasheria kali, nakumbuka mwaka jana kulikuwa na gumzo kubwa hapa China baada ya serikali kuboresha sheria ya haki za wateja, na kuhakikisha kuwa mtu yoyote anayefanya ujanja au ulaghai kwa mteja anachukuliwa hatua kali. Kwa hiyo jibu ni kuwa, wenzetu wana sheria na kuna utaratibu mzuri wa kusimamia na kutekeleza sheria hizo.

    Fadhili: Nakumbuka hiyo sheria ya kulinda haki za mteja ilizungumzwa sana mwezi Oktoba mwaka jana. Ninachokumbuka sana ni kuwa sheria ilisema kama ukimuuliza mtu bidhaa isiyo na ubora, au bidhaa feki ambayo mtu atailalamikia, kama ikithibitishwa basi maana yake ni kuwa kwanza unalipa fidia, yaani pesa zote alizolipa mteja, pili ni unalipa gharama za usumbufu ambazo zinaweza kuwa kubwa kuliko hata bei ya bidhaa, na tatu unatakiwa kulipa faini ya kufanya udanganyifu, na baada ya hapo unaweza hata kufikishwa mahakamani. Kwa hiyo kimsingi sheria hii ndio inayowalinda wateja wa hapa China, na ndio maana ukienda supermarket huwezi kukuta bidhaa feki.

    Pili: Lakini mbali na hili serikali pia ina utaratibu fulani ambao naweza kusema ni njia ya kupambana na tatizo kutoka kwenye chanzo. Viwanda vinavyozalisha bidhaa, kwanza vinatakiwa vithibitishwe kuwa vina uwezo huo, na kama vikiwa na uwezo huo kuna idara inayoitwa Idara ya kuthibitisha ubora wa bidhaa. Kama ukiangalia bidhaa nyingi za hapa China unaweza kuona kuna maneno yanayosomeka "Quality Control Approved" kwa hiyo kabla ya bidhaa kutoka kiwandani kuna namna mbili ya kuhakikisha kuwa ubora wake unakaguliwa.

    Fadhili: Labda wasikilizaji wanaweza kujiuliza, sasa kama kuna utaratibu kama huu inakuwaje bidhaa feki kutoka China zinafika Tanzania au Kenya? zinatoka wapi? Tatizo ni kuwa hapa China wenzetu wana teknolojia nzuri kwa hiyo kuna wakati bidhaa zinatengenezwa kwenye vijiwanda ambavyo vimefichwa, na kumewahi kuwa na habari kuwa wengine wanatengeneza kwenye meli ambazo zinazokaa mbali baharini ambako wakaguzi hawawezi kufika kurahisi, na kama zikisafirishwa kwenye katika nchi nyingine zinasafirishwa juu kwa juu.

    Pili: Kwa hiyo tukiangalia kwenye nchi zetu kama Tanzania unaweza kuona kuwa kuna dosari fulani kwenye uagizaji wa bidhaa na uuzaji wake na hata usimamizi wa sheria zinazohusu ubora wa bidhaa.

    Pili; Naona tatizo kubwa lipo kwenye usimamizi wa sheria, labda kuwakumbusha wasikilizaji ni kuwa, sheria za hapa China kweli ni kali. Kuna sheria nyingine ambayo inasema, kama ukiuza bidhaa feki au mbovu ambayo ikasababisha ulemavu au hata kifo cha mtu, basi adhabu ya kwanza ni kulipa faini na fidia kutokana na madhara yaliyotokea, lakini kingine ni kuchukuliwa hatua za kisheria. Sheria hizi kidogo hazisimamiwi vikali katika baadhi ya nchi.

    Fadhili: Lakini kuna baadhi ya matatizo pia yanawakumba wateja wa hapa China, ambayo bado hujaingia kwenye nchi za Afrika. Na kama yameingia basi yatakuwa ndio yanaanza kuingia kwa sasa. Hapa China kwa sasa biashara ya mtandao wa internet imekuwa kubwa, mtu anaweza kutuma bidhaa kutoka Guangzhou wewe unaishi Beijing, na unalipa kwa njia ya mtandao wa internet. Kwanza kuna uwezekano ukatumiwa bidhaa ya ovyo, na inawezekana kuna uwezekano kuwa ukalipia hela zako zikapotea na usimpate muuzaji, hizi ni changamoto ambazo wateja hapa China wanakabiliwa nazo.

    Pili: Lakini pia sheria ya kulinda mteja pia ina vipengele vya kuwalinda wateja wanaonunua bidhaa kwenye mtandao wa internet. Kwa mfano sheria inasema kama bidhaa ni mbovu, mnunuzi anaweza kurudisha na kudai hela zake, lakini anatakiwa kufanya hivyo ndani ya siku 7. Na mteja ana haki kabisa ya kukataa bidhaa feki, na hapa China wateja wakikataa bidhaa muuzaji anarudisha pesa, muuzaji hawezi kusema ukinunua basi huwezi kurudisha.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako