• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wathamini mambo ya jadi kwa kutumia teknolojia za kisasa

    (GMT+08:00) 2014-03-26 14:31:08
    Katika miaka ya hivi karibuni hali ya maisha imeonekana kubadilika kwa kasi, kuna mambo mengi ya kisasa yameingia katika maisha yetu, na baadhi yetu tumeanza kupuuza yale mazuri ya jadi tukiyaona ya kishamba, na kukumbatia zaidi mapya tunayoita ya kisasa. Lakini hapa China wenzetu wanafanya mambo ya maana sana, kuthamini mambo ya jadi kwa kutumia teknolojia za kisasa.

    Pili: China inasifika kuwa na utamaduni wa zaidi ya miaka 5000, na katika miaka hiyo elfu tano kuna mambo mengi sana ambayo baadhi ya watu wanaweza kusema yamepitwa an wakati na baadhi ya watu wanaona ni mambo ambayo yanatakiwa kuhifadhiwa na hata kufahamishwa kwa watu. Lakini jambo la muhimu ni kuwa China ya sasa ni nchi ya teknolojia, matumizi ya teknolojia yamekuwa makubwa sana, na baadhi ya watu hasa vijana wanaona kuwa ya zamani yakae pembeni na sasa tuchangamkie haya ya kisasa. Lakini wengine wanaona kuwa ya zamani, hayatakiwa kutupwa kwa kuwa tuna mapya, kwa hiyo ni bora mapya na ya zamani yachanganywe.

    Fadhili; Ukitaka kujua mambo haya unaweza kuangalia mfano wa mtoto. Zamani sisi tulipokuwa watoto tulikuwa tunachezea magari ya waya, au tulikuwa tunatengeneza ndege za mabua, lakini siku hizi watoto wanataka michezo ya kompyuta na michezo kama PSP, ile ambayo sisi tulikuwa tunachezea wanaona ni ya kishamba. Hapa China wenzetu wanachofanya ni kuwa michezo ile ile ya zamani, sasa inafanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

    Pili: lakini wakati fulani tunaweza kusema kuwa watu wamechoka kujifunza kwa kutumia njia za zamani, kwa hiyo ili wasiache kabisa kujifunza, ni vizuri kutumia njia wanazopenda ili wajifunze kwa urahisi.

    Fadhili: Naweza kusema siku hizi kuna njia nyingi sana za kujifunza, labda mtu uwe mvivu sana na usijue kila kitu, lakini kama kweli unapenda kujifunza na unaweza kusoma na kusikia, ukipanda basi, subway au hata kutembea mjini unaweza kuona kitu ambacho kinavutia kuliko kitabu, au unaweza kusikia kitu ambacho kiavutia kuliko kumsikiliza mwalimu darasani.

    Pili: Hapa China kuna mambo mengi sana ya jadi na ya kale. Kwa mfano kuna majumba ya kihistoria, ala za muziki na hata vyakula vya jadi. Na kama ulivyosema ukiangalia kwa upande mwingine kila unapopita na kila unapokwenda unaweza kuona mambo ya kisasa. Kwa hiyo kutembea na kuangalia tu, na hata kupata fursa ya kusikiliza unaweza kuwa na fursa nzuri ya kujifunza mambo ya sasa na hata ya zamani. Na uzuri ni kuwa hata kwa watu ambao ni wavivu kutembea unaweza kujifunza ukiwa nyuymbani, njiani au hata kataika sehemu ya mapumziko. Kwa mfano kwa sasa kuna hii application ya mawasiliano ya kijamii ya WeChat, ambayo vijana wengine wa China wanaipenda, kwa hiyo wataalamu walichofanya ni kujaribu kuihusisha hiyo application na mambo ambayo vijana wanaona ni ya kale.

    Fadhili: Mfano mzuri ambao hata mimi naweza kusema nimefurahia, ni wa jumba ka kifalme la Beijing, ambalo ni maarufu kwa jina la Forbidden City. Hili ni jumba la zamani sana, lilijengwa miaka 500 iliyopita., Baadhi ya vijana wanaona ah hili jengo la zamani sana na lipo kila siku, lakini kwa kutumia hiyo application ya weChat unaweza kuangalia na kusoma baadhi ya mambo kuhusu jumba hilo hata bila kwenda. Kuna majumba mengi ya makumbusho hapa China ambayo yanatumia mbinu kama hiyo

    Pili: Lakini wenzetu naweza kusema wanafanya vizuri zaidi kwa kuwa utamaduni wao licha ya kuwafundisha watoto nyumbani, pia wanawafundisha shuleni. Kwa kuwa kwa sasa wanazingatia mambo ya kisasa na kuna njia za kisasa za kufundishia, watoto wanaweza kujifunza na kusoma kwa njia za kisasa. Uzuri ni kuwa kutokana na teknolojia ya kufundisha kutoka mbali, watoto walioko kilometa 5000 kutoka Beijing ambao hawana uwezo wa kuja Beijing, sasa wanaweza kuona picha au hata video.

    Fadhili: siku hizi watu wanasema teknolojia imepunguza umbali, lakini ukweli ni kuwa hata ugumu wa kujifunza kwa sasa umepungua kutokana na kuwa na mbinu nyingi za kisasa za kujifunza.

    Pili: Naweza kutoa mfano mwingine, siku hizi kutokana na matumizi ya computer hapa China kuna baadhi ya watu wanashindwa kuandika kwa kutumia kalamu. Hasa wale wanaofanya kazi na kompyuta kila siku, hata kama wanajua labda wameanza kusahau, kwa hiyo ili kuwafanya watu wasisahau baadhi ya makundi ya watu wanaandaa shughuli za kuwashindanisha watu kuandika kwa kutumia kalamu, na wachina wana uandikaji fulani wa maandishi ya kichina. Kwao ni sanaa, lakini vijana wanaona ni kitu kisicho na maana.

    Fadhili: Lakini kitu kingine ambacho wenzetu wachina ni hodari ni kujitahidi kutumia njia zote kulinda utamaduni wao na kulinda jadi zao. Kwa mfano hapa China kwa miaka karibu 5000 sasa sikukuu ya Spring ndio sikukuu kubwa kwa wachina, na hii haibdiliki licha ya kuwepo kwa maendeleo makubwa duniani na sherehe nyingi mbalimbali. Wameweka sheria ambazo zinahakikisha kuwa sikukuu za jadi hazisahauliwi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako