• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liverpool yaipiku Chelsea katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuadhibu Tottenham Hotspurs

    (GMT+08:00) 2014-04-01 15:24:24

    Liverpool imejikita kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuiadhibu Tottenham hotspurs 4-0 katika mechi iliyosubiriwa na wengi katika uwanja wa Anfield. Ushindi huo sasa umeifanya Liverpool kurejea kileleni kwa alama 71 mbili zaidi ya wapinzani wao wa karibu Chelsea .

    Hivi sasa Manchester United inaiongoza Manchester City, kwa alama nne licha ya vijana hao wa Manuel Pellegrin kuwa na mechi mbili zaidi za kucheza . Man City na Chelsea bado watakabiliana na vijana wa mkufunzi Brendan Rodgers Liverpool katika uga wa Anfield. Kama watashinda mechi hizo basi Liverpool itajiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989-90. Arsenal ni ya nne kwa alama 64. Everton ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham inafunga orodha ya tano bora kwa alama 60.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako