• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahasimu wa Hispania Atletico Madrid na Barcelona watoka sare ya 1-1 kwenye mkondo wa kwanza wa robo fainali za klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2014-04-03 14:37:53

    Vita vya mahasimu wa nyumbani Atletico Madrid na Barcelona viliishia sare ya nne msimu huu baada ya timu hizo mbili za Uhispania kutoka sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza wa ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyozaragazwa katika uga wa Camp nou. Atletico inayoongoza katika dimba la nyumbani ya la Liga, sasa imejipatia bao muhimu la ugenini licha ya kufuzu kuingia katika robo fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1997. Licha ya barcelona kupigiwa upatu kushinda taji hilo, Atletico ndio walkuwa wa kwanza kutikisa wavu kupitia kiungo wake Diego aliyechukua nafasi ya Diego Costa aliyelazimika kuondolewa uwanjani baada ya kupata jeraha katika dakika ya 30. Licha ya ulinzi mkali wa Atletico, Barca ilijifurukuta na kufunga kupitia kijana matata wa Brazili Neymar aliyesawazisha zikiwa zimesalia dakika 20 mechi hiyo kukamilika. Juhudi za Barcelona za kutafuta bao la Ushindi ziliambulia patupu kwani ngome ya ulinzi ya Atletico ilikuwa kali mno.Hivi sasa Athletico inaongoza ligi ya nyumbani kwa alama moja zaidi ya Barca

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako