• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais Xi Jinping barani Ulaya yahimiza maendeleo ya uchumi na biashara kati ya China na Ulaya

    (GMT+08:00) 2014-04-09 20:45:14

    Kuanzia tarehe 22 mwezi Machi hadi tarehe 1 mwezi huu, rais Xi Jinping wa China alihudhuri mkutano wa tatu wa wakuu wa usalama wa nyukilia uliofanyika huko Hague nchini Uholanzi, kufanya ziara nchini Uholanzi, Ufaransa, Ujerumani na Belgium, na kutembelea makao makuu ya shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa na makao makuu ya Umoja wa Ulaya. Tarehe 2 serikali ya China imetoa waraka wa sera za China kwa Ulaya, ambao umeweka mpango wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika miaka 5 hadi 10 ijayo. Rais Xi amesisitiza kuwa, lengo la China ni kuifanya thamani ya biashara kati ya China na Ulaya ifikie dola za kimarekani bilioni 1,000 mwaka 2020.

      Wakati alipohutubia katika chuo cha Ulaya cha Bruges, rais Xi Jinping amesema kuna fursa kubwa katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya. Amesema hivi sasa China na Ulaya zote ziko kwenye kipindi muhimu cha maendeleo, zinakabiliwa na fursa na changamoto ambazo hazikuwepo zamani, na China inapenda kushirikiana na marafiki wa Ulaya na kujenga darasa la urafiki na ushirikiano kati ya Asia na Ulaya.

    Rais Xi Jinping amezitaka China na Ulaya zishikilie kufungua mlango kwa pamoja, kuharakisha mchakato wa mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji, na kujadili ujenzi wa eneo la bishara huria, ili kutimieza lengo la kuifanya thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ifikie dola za kimarekani bilioni 1000 hadi mwaka 2020.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa na Umoja wa Ulaya, thamani ya biashara kati ya China na Ulaya mwaka jana ilifikia dola za kimarekani bilioni 658, hii inamaanisha kuwa, hadi mwaka 2020, biashara kati ya pande hizo mbili itaongezeka kwa asilimia 52. Umoja wa Ulaya ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa China, na China ni mwenzi mkubwa wa pili wa biashara wa Umoja wa Ulaya. Kutokana na takwimu zilizotolewa na kamati ya Ulaya, kila mwaka thamani ya biashara kati ya China na Ulaya inazidi dola za kimarekni bilioni 588.6, ambayo ni sawa na bilioni 1.6 kila siku.

       Mwanauchumi Bw. Tom Orlik amesema, uhusiano wa biashara ni muhimu sana kwa China na Ulaya. Barani Ulaya wateja wananufaika kutokana na bidhaa za elekroniki na nguo zenye gharama nafuu zinazotengenezwa na China. Nchini China, wateja wananufaika kutokana na bidhaa za sayansi na teknolojia za juu, na kuongezeka kwa wateja wa China kumepanua soko kwa chapa za anasa za Ulaya. Diplomasia ya kiuchumi imehimiza uhusiano wa biashara, ambayo imepunguza vikwazo dhidi ya usafirishaji wa bidhaa na huduma, na kuzinufaisha China na Ulaya.

      Kampuni ya MSI ya Marekani imeona kuwa, wawekezaji wanaweza kuwekeza zaidi kwenye kampuni za China, au kuwekeza kupitia wenzi wa ushirikiano wa kampuni za China na wasambazaji wao katika nchi nyingine.

      Katika kipindi cha ziara yake, rais Xi Jinping alitembelea bandari ya Duisburg nchini Ujerumani, ambayo ni kituo cha mwisho cha reli ya kimataifa kutoka Chongqing hadi Ulaya ambayo itapitia mkoa wa Xinjiang. Ingawa ni mbali sana, lakini treni inayoendeshwa kwa kampyuta na vifaa vya elektroniki inaweza kutumia siku 16 tu kufika Duisburg kutoka Chongqing nchini China. Msemaji wa bandari ya Duisburg Bw. Julian Pork amesema, reli hiyo inaitwa kuwa njia mpya ya hariri nchini China, ambayo itatoa mchango mkubwa kwa biashara kati ya China na nchi husika. Rais Xi Jinping amesema, China imetoa mwito wa kujenga eneo la uchumi la njia ya Hariri, na inashikilia wazo la kupata maendeleo ya pamoja, kuunganisha soko la Asia na Ulaya, na kuwanufaisha watu wa nchi zilizoko kwenye njia hiyo.

    Mtafiti wa taasisi ya ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na kibiashara ya wizara ya biashara ya China Bw. Mei Xinyu amesema, eneo la uchumi la njia ya Hariri litahimiza maendeleo ya Asia ya Kati, Russia, Ulaya Mashariki, Ulaya Kusini na sehemu husika za Ulaya Magharibi, pia linaweza kuzifanya sehemu nyingi zaidi zinufaike na maslahi ya maendeleo ya uchumi na biashara kati ya China na Ulaya. Kwa biashara kati ya China na Ulaya, ujenzi wa eneo hilo unasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na kupunguza hatari ya usafirishaji.

    Mei Xinyu amesema, ili kujenga eneo la uchumi la njia ya Hariri kwa taratibu, ni lazima kuweka mazingira ya amani na utulivu kwa maendeleo ya uchumi na jamii, kulinda na kukuza reli, barabara, safari za ndege za kimataifa, kujenga na kukamilisha miundo mbinu ya nchi za Asia Kati, na kuendeleza mambo ya usafirishaji na miundo mbiunu ya telekom na umeme. Bw.Mei Xinyu amesema, kujenga na kukamilisha mfumo wa usafirishaji ni muhimu sana, kwani mfumo huo ni sharti la kwanza la maendeleo ya uchumi. Hii inaweza kuboresha hali isiyoridhisha ya China katika biashara za huduma za usafirishaji wa kimataifa.

      Kutokana na waraka wa sera za China kwa Umoja wa Ulaya, pande hizo mbili zitahimiza ongezeko la kasi la mazao ya kilimo, kuzidisha ushirikiano kati yao kwenye sekta ya nishari, kutilia maanani ushirikiano kwenye eneo la usafiri wa anga, kuhimiza ujenzi wa vituo vya utafiti wa pamoja, na kuimarisha mawasliano na ushirikiano kati yao kwenye safari za ndege za abiria.

    Uchumi wa Afrika Mashariki waongezeka kwa kasi zaidi barani humo

    Mkutano wa 7 wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa na kamati ya Umoja wa Afrika umefanyika hivi karibuni huko Abuja nchini Nigeria. Ripoti iliyotolewa na mkutano huo inasema, ongezeko la uchumi wa Afrika Mashariki katika mwaka jana limefikia asilimia 6, hasa katika nchi za Rwanda na Tanzania, ambako ongezeko la uchumi wa nchi hizo limefikia asilimia 7.4 na 7.2. Ripoti hiyo pia imekadiri kuwa, mwaka huu ongezeko la uchumi wa Afrika Mashariki litafikia asilimia 7, na Afrika Mashariki itakuwa sehemu yenye ongezeko la kasi zaidi barani Afrika.

    Ripoti hiyo inasema, uwekezaji wa Afrika Mashariki, hasa katika sekta za madini zikiwemo mafuta na gesi unaongezeka kwa kasi sana. Mwaka huu mwelekeo mzuri wa ongezeko la uchumi wa kanda hiyo umewavutia wawekezaji wengi. Utulivu wa bei ya nafaka kutokana na ongezeko la uzalishaji wa nafaka umesaidia nchi husika kudhibiti mfumuko wa bei. Mwaka jana mfumuko wa bei wa nchi za Afrika ulipungua, kwa mfano, katika miaka miwili iliyopita, mfumuko wa bei nchini Kenya ulifikia asilimia 5.5, na kwa Rwanda ulifikia asilimia 4.58 tu.

      Ripoti pia inasema, ongezeko la usafirishaji wa bidhaa kwa nje pia limechangia ongezeko la uchumi wa Afrika Mashariki. Ripoti hiyo inakadiri kuwa, mwaka 2014 thamani ya jumla ya usafirishaji wa bidhaa nje ya bara la Afrika itapungua, lakini thamani ya usafirishaji wa bidhaa kwenye kanda ya Afrika Mashariki itaongezeka, kwa sababu usafirishaji wa bidhaa zisizo za jadi katika nchi za sehemu hiyo utaongezeka, kwa mfano wa usafirishaji wa maua na biashara za huduma kati ya Kenya, Tanzania na Ethiopia. Licha ya hayo, utumaji wa fedha kutoka nchi nyingine pia ni sababu nyingine inayohimiza ongezeko la uchumi wa Afrika Mashariki. Mwaka 2013 thamni ya huduma hiyo barani Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 70. Katika siku za baadaye, huduma hiyo itaendelea kuwa nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya Afrika, ikiwemo Afrika Mashariki.

      Ingawa Afrika Mashariki imedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi, lakini wanauchumi pia wameeleza matatizo ya maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Kwanza, miundombinu mibaya na vikwazo vya biashara bado ni tatizo kuu la uwekezaji na ongezeko la uchumi katika nchi za Afrika Mashariki. Wanauchumi wamependekeza kuwa, nchi mbalimbali za sehemu hiyo zinapaswa kuharakisha mchakato wa utandawazi wa uchumi, kuondoa vikwazo mbalimbali vya biashara, ili watu, fedha na huduma ziweze kusafiri katika nchi mbalimbali za sehemu hiyo.

    Licha ya hayo, ingawa hali ya siasa ya nchi nyingi za Afrika Mashariki ni tulivu, lakini nchi kadhaa za sehemu hiyo na nchi jirani zinakabiliwa na migogoro. Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini zinakabiliwa na msukosuko wa ndani, mgogoro wa mipaka kati ya Sudani na Sudan Kusini bado haujatatuliwa, na kundi la Al Shabaab la Somalia na hali mbaya ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zote zinatishia usalama na utulivu wa Afrika Mashariki. Wanauchumi wameonya kuwa, hivi sasa migogoro ya sehemu jirani haiathiri sana maendeleo ya uchumi wa Afrika Mashariki, lakini watu wanapaswa kufuatilia athari zaidi zitakazoletwa kutokana na kuongezeka kwa migogoro hiyo.   

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako