• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na nchi za nje yashuka katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2014-04-11 18:00:33

    Takwimu mpya zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonyesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilipungua kwa asilimia 3.7 na kufikia dola za Kimarekani bilioni 949.9, ikilinganishwa mwaka jana kipindi kama hicho.

    Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa nje ya China ilipungua kwa asilimia 6.1 na kufikia dola za kimarekani bilioni 483, huku thamani ya uingizaji bidhaa nchini ikiwa ni bilioni 466.9, ambazo ni pungufu kwa asilimia 1.2. Hali hii imepelekea kupungua kwa urari wa kibiashara kwa asilimia 60.9 kulika mwaka jana kipindi kama hicho. Mtaalamu wa Kituo cha Taifa cha Taarifa cha China profesa Yan Min anaona bei ndogo ya bidhaa zinazouzwa kwa wingi katika masoko ya kimataifa inatishia uingizaji wa bidhaa nchini China. Anasema kuongezeka kwa thamani ya sarafu ya RMB na hali mbaya ya maendeleo ya uchumi wa makundi ya kiuchumi yaliyoibuka hivi karibuni kumeathiri vibaya uuzaji bidhaa za China katika nchi za nje.

    (sauti 1)

    "Uchumi wa Russia unayumbayumba kufuatia kuongezeka kwa hatari ya siasa za kijiografia. Kasi ya ongezeko la uchumi wa Brazil na Afrika Kusini inapungua kutokana na kushuka kwa uuzaji wa bidhaa zinazouzwa kwa wingi zaidi katika masoko ya kimataifa. Madeni ya India yanaongezeka, hali ya mambo ya fedha inakabiliwa na shida kubwa na muundo wa uchumi umekwamisha ukuaji wa uchumi wake. Hali hiyo imeathiri vibaya ongezeko la uuzaji wa bidhaa za China nje ya nchi."

    Akizungumza na waandishi wa habari, wakuu wa makampuni ya kauri ya Huafumei na Guang Xi Sanhuan wanasema hali ya uuzaji wa bidhaa za kauri si nzuri kufuatia kushuka kwa mahitaji nje ya nchi. Wanasema, (sauti 2) "Hali ya uuzaji wa bidhaa inaathirika kiasi, kwani uchumi wa dunia bado ni dhaifu." "hali ya uuzaji wa bidhaa zetu nje ya nchi inaathiriwa na mazingira ya kimataifa, uchumi wa dunia uko vipi, pia tujiulize uuzaji wetu ukoje."

    Ingawa biashara kati ya China na nchi za nje ulishuka katika robo ya kwanza ya mwaka huu, msemaji wa Idara Kuu ya Forodha Bw. Zheng Yuesheng anaona hii ni kwa muda tu, kwa kuwa biashara hiyo bado iko katika hali inayokubalika.

    (sauti 3) "katika robo ya kwanza, biashara kati ya China na nchi za nje ilishuka, haswa uuzaji nje bidhaa ambao ulishuka kwa kiasi kikubwa zaidi, hii imeonesha kuwa biashara ya nje ya China imepata pigo kidogo, lakini baada ya kuondoa sababu zilizoathiri takwimu za mwaka jana kipindi kama hicho, tunaona biashara kati ya China na nchi za nje bado iko katika hali inayokubaliwa."

    Kwa mujibu wa takwimu za awali za kiuchumi, biashara kati ya China na nchi za nje itaongezeka kuanzia mwezi wa tano na kuingia kwenye kipindi cha ukuaji wa pole pole. Bw. Zheng anasema,

    (sauti 4)

    "Takwimu za awali za kiuchumi zimeonesha kuwa biashara kati ya China na nchi za nje itapanda katika miezi miwili na mitatu ijayo, na inakadiriwa kuwa katika robo ya pili ya mwaka huu, ongezeko hilo litaizidi ile ya robo ya kwanza."

    Bw. Zheng ameongeza kuwa ushindani wa biashara ya China na nchi za nje pia unapungua kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa nchi na sehemu zilizoko karibu na kuongezeka kwa mikwaruzano ya kibiashara na wenzi wakubwa wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako