• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia zinapaswa kupanua zaidi ushirikiano halisi kwenye msingi wa uaminifu wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2014-04-15 19:47:13


    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje ya Russia ambaye yuko ziarani nchini China Bw. Sergei Lavrov. Rais Xi Jinping amesema, uhusiano kati ya China na Russia uko katika kipindi kizuri zaidi katika historia, na nchi hizo mbili zinapaswa kutumia fursa hiyo kupanua zaidi ushirikiano halisi kwenye msingi wa uaminifu wa kisiasa. Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Russia si kama tu unanufaisha nchi hizo mbili, bali pia una umuhimu mkubwa kwa amani na utulivu wa dunia. China na Russia zinatakiwa kuendelea na mawasiliano ya kimkakati, kuungana mkono zaidi katika mambo ya kisiasa, kuharakisha ushirikiano wa miradi mikubwa ya kimkakati, na kuimarisha ushirikiano katika mambo ya kimataifa na kikanda. Bw. Lavrov amesema, Russia inapenda kuendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yake na China. Ameongeza kuwa, rais Vladmir Putin wa Russia anatarajia kufanya ziara nchini China na kuhudhuria mkutano wa wakuu kuhusu kujenga uaminifu na kukuza ushirikiano barani Asia utakaofanyika mjini Shanghai.
    Naye waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi leo baada ya kukutana na Bw. Lavrov amewaambia waandishi wa habari kuwa, China itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa mkutano wa hatua za ushirikiano na uaminifu barani Asia CICA mwaka huu hadi mwaka 2016. Amesema wakati wa mkutano wa wakuu wa CICA, China itazihimiza nchi mbalimbali ziunde mtizamo mpya wa usalama barani Asia, na kujadili kuundwa kwa utaratibu mpya wa kuhusu usalama na ushirikiano barani Asia.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako