• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukraine yafanya operesheni ya kijeshi katika sehemu ya mashariki

    (GMT+08:00) 2014-04-16 10:50:58

    Kutokana na maandamano yanayofanywa na watu wanaoiunga mkono Russia mashariki mwa Ukraine yaliyoanza tarehe 6 mwezi huu, jana Ukraine ilianza kufanya operesheni ya kijeshi katika sehemu ya mashariki. Hatua hiyo inafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Rais Vladmir Putin wa Russia jana aliongea na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa simu na kusisitiza kuwa, Russia inatarajia Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa watailaani Ukraine kwa kukiuka katiba. Bw. Ban Ki-moon amesema, kwa sasa hali ya sehemu ya mashariki mwa Ukraine si tulivu, amezitaka pande mbalimbali zichukue hatua mara moja ili kupunguza hali ya wasiwasi.

    Vilevile, rais Putin pia alipoongea na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amesema msukosuko wa Ukraine unapamba moto, na kuifanya nchi hiyo inakaribia kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    Tofauti na msimamo wa Russia, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bibi Jen Psaki ameitetea hatua ya serikali ya Ukraine akisema serikali ya Ukraine imelazimika kujibu uchochezi uliofanywa na watu wenye silaha mashariki mwa nchi hiyo. Pia alikanusha kauli kuwa Ukraine imeanza vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kusema Ukraine imetuma jeshi kwa lengo la kutuliza hali na kulinda amani ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako