• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana na China wasanifu vitu vya kitalii vya mitindo ya kipekee

    (GMT+08:00) 2014-04-16 14:02:25

    Vitu vya kitalii vinakosolewa na watalii mara kwa mara kutokana na sifa mbaya na sura zinazofanana. Lakini siku hizi katika miji mingi yenye vivutio vya utalii nchini China ikiwemo Jindezheng, Dunhuang na Xi'an, vijana wanaozaliwa katika miaka ya 80 au 90 karne iliyopita wamesanifu vitu vya kitalii vya mitindo mipya.

    Gulio la vyombo vya kauri linafanyika kila jumapili asubuhi katika kiwanda cha sanamu na vyombo vya kauri cha Jindezheng. Wanafunzi wengi wanaosoma katika chuo cha kauri cha Jindezheng na vijana wanaotengeneza vyombo vya kauri wanauza bidhaa zao zenye sifaa ya kipekee kwenye gulio hilo.

    Vyombo hivi ni pamoja mabuli, vyungu vya maua, sahani na mabakuli, lakini vina mitindo ya kipekee kutokana na michoro na makumbo tofauti. Wanunuzi pia wanaweza kununua mifuku, bangili, bizimu, vyombo vya kuwekea sabuni, vioo na vyombo vya kuwekea kadi vya kauri katika gulio hilo.

    Bw. Feng Jiange kutoka mji wa Beijing anayeshughulikia usanii alinunua vitu vingi kutoka gulio hilo. Alisema karibu vitu vyote vinavyouzwa katika gulio hilo vinasanifiwa na wasanii kwa kujitegemea, si kama tu ni rahisi kutumiwa, bali pia vina mitindo ya kipekee. Watu wachache tu waliotembelea gulio hilo hawakununua bidhaa yoyote. Bw. Gong Fu kutoka mkoa wa Hunan hata alinunua makumi ya vikombe ili kuwazawadia marafiki zake.

    Habari zinasema vitu vingi vya kitalii vinatengenezwa kwa wingi na viwanda vidogovidogo, hivyo bidhaa zenye sifa za kipekee, zinazostahili kuhifadhiwa na zinazosanifiwa na wasanii kwa kujitegemea ni chache. Lakini vitu vya kitalii vinavyosanifiwa na vijana hao vimeanza kubadilisha hali hii, na vinavutiwa na wateja wengi.

    Bi. Yang Yang aliyehitimu kutoka chuo kikuu aliamua kuanzisha shughuli zake nyumbani mjini Dunhuang. Alianzisha duka dogo la Yangkeboluo kwenye gulio la usiku, ambalo linauza vitu vya kitalii vinavyosanifiwa naye vikiwemo ramani za mji wa Dunhuang zenye mtindo wa mchoro, mitandio ya hariri iliyochapishwa ramani za Dunhuang na kadi za michoro.

    Bi. Yang Yang anapenda kufanya utalii na aliwahi kutembelea miji mingi nchi China. Aligundua kuwa vitu vya kitalii katika miji mbalimbali vinafanana sana, hivyo aliamua kutengeneza vitu ambavyo vinapatikana mjini Dunhuang tu.

    Lakini kusanifu vitu vya kitalii vya kipekee si kazi rahisi. Ili kuchora ramani nzuri, Bi. Yang alitumia miezi mitano kutembelea mitaa na mikahawa mbalimbali mjini Dunhuang. Na mitandio yake pia ilisanifiwa na msanifu maalum na kutengenezwa huko Hangzhou. Kutokana na juhudi zake kubwa, bidhaa zake zinapendwa na kusifiwa na wateja.

    Mteja mmoja Zhang Qin alisema alipoona kadi na mitandio hiyo, alifurahi sana, ametembelea gulio la usiku kwa muda mrefu, na mwishowe aligundua bidhaa zinazostahili kununuliwa.

    Maduka ya vitu vya kitalii vinavyosanifiwa na wasanifu kwa kujitegemea pia yanaonekana mijini Xi'an na Chengdu. Duka la Sanrenli lililoko katika mtaa wa wakazi wa kabila la Wahui linauza beji, kadi na mapambo madogo yanayowekwa kwenye mlango wa jokofu ambayo yamechapishwa lafudhi ya mkoa wa Shaanxi. Na katika duka la "nyumba ya panda" lililoko mjini Chengdu, wateja si kama tu wanaweza kununua vitu vya kuwachezea watoto vya panda vinavyovaa nguo mbalimbali, bali pia wanaweza kununua balkuli, vijiti, viatu, kofia, mitandio na mifuko yenye michoro ya panda.

    Sasa Bi. Yang Yang anayeuza vitu vya kitalii huko Dunhuang anaongoza wafanya kazi kadhaa, wakiwemo wasanifu wanne na wauzaji watatu. Tofauti na mji wa Jindezheng, watu wanaoshughulikia usanifu wa vitu vya kitalii kama Yang Yang ni wachache sana. Tatizo hili pia liko katika miji mingine mingi.

    Ukiukaji wa haki ya kunakili pia ni tatizo linalowasumbua vijana wanaosanifu vitu vya kitalii.

    Mwandishi wetu wa habari alipowahoji wasanifu mjini Jindezheng, wasanifu wengi walisema tatizo la ukiukaji wa haki ya kunakili ni kubwa. Bw. Shao anayeuza kikombe kinachosanifiwa naye alisema angetoa bidhaa mpya wiki hii, bidhaa zinazofanana zingekuwa zitauzwa hapa na pale sokoni wiki ijayo.

    Bw. Yang Yang pia aliwahi kusumbuliwa na ukiukaji wa haki za kunakili. Alisema siku moja aliona kadi za chapa tofauti zenye michoro iliyo sawa na kadi zake, alikasirika sana. Ingawa alijua tatizo hili zamani, lakini hakufikiri kuwa atasumbuliwa na tatizo hilo baada ya muda mfupi tu tangu aanze shughuli zake.

    Ili kukabiliana na tatizo hili, vijana hawa wameharakisha kusanifu bidhaa mpya na kuzifanya bidhaa zao kuigwa na wengine lakini kutoshindwa na bidhaa za wengine. Wanawatarajia watu wengi zaidi kushiriki kwenye kazi zao, kuunda shirika la wasanifu na kutunga kanuni mbalimbali, pia wanaitarajia serikali itawafuatilia na kutoa uungaji mkono zaidi, na kulinda haki zao za kunakili kwa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako