• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfanyabiashara wa Taiwan anyeshughulikia mambo ya kilimo ya kiwango cha juu katika China bara

    (GMT+08:00) 2014-04-16 14:02:48

    Kila ifikapo majira ya spring, miti ya pea inachanua katika mashamba ya pea ya kampuni ya kilimo cha kiwango cha juu ya Shangkunshi ya mji wa Kunshan, mkoani Jiangsu, China. Maua ya kupendeza yanawavutia watalii wengi katika siku za mapumziko. Meneja mkuu wa kampuni hiyo ambaye ni mfanyabiashara kutoka kisiwa cha Taiwan Bw. Huang Xuheng alisema kampuni yake inafungua mlango kwa watalii, anapenda kushughulikia kilimo kwa sababu kilimo ni mambo yanayohitaji watu kuhisi mwenyewe katika mazingira ya kimaumbile.

    Bw. Huang anaonekana kuwa mwanachuo badala ya mfanyabiashara. Katika miaka 11 iliyopita, Bw. Huang mwenye shahada ya uzamivu ya saikolojia ya Chuo kikuu cha Harvard alikuwa mwalimu wa Chuo Kikuu cha Yangming cha Taiwan.

    Alipoambatana na baba na rafiki yake kukagua mradi wa ufugaji wa kama mjini Kunshan, aligundua kuwa mji huo una hali nzuri ya kijiografia, mazingira mazuri na ardhi nzuri, hivyo alikuwa na mpango wa kushughulikia kilimo mjini humo.

    Alisema kila mtu anahitaji kula chakula kila siku, hivyo siku zote kilimo kina mustakabali mzuri. Mambo ya kilimo pia yanaweza kuwa shughuli za kiwango cha juu kutokana na matumizi ya teknolojia mbalimbali za kisasa ikiwemo teknolojia ya Internet.

    Alipozungumzia sababu ya kushughulikia kilimo cha pea, alisema kwa sababu baba yake anapenda kula pea, anataka kuzalisha mapea yenye sifa nzuri kwa baba yake.

    Bw. Huang alisema anaona kilimo ni mambo ya kuvutia, kwa sababu anaweza kuona maua yanachanua katika majira ya spring na kuvuna matunda katika majira ya autumn; lakini kilimo pia ni kazi ngumu, kwa sababu anatakiwa kuzalisha matunda yenye sifa nzuri ili kuwajibika na afya ya umma. Hivyo kampuni yake inazalisha matunda ya kiwango cha juu kwa kutumia teknolojia za hali ya juu tangu ianzishwe. Kwa mfano, kampuni hiyo inauruhusu mti mmoja wa pea wenye umri wa miaka mitatu kuzalisha mapea 36, ili kuhakikisha sifa nzuri; na pia inatumia mbolea zisizo za kemikali zenye bei ghali, ambazo zinaiwezesha miti kuzalisha mapea matamu.

    Kampuni yake ina kazi nyingi katika majira ya spring, ambayo zinahusiana na mavuno ya mwaka huu. Licha ya kampuni yake mjini Kunshan, kampuni yake pia yana matawi zaidi ya 20 katika China bara. Hivi karibuni Bw. Huang anakwenda sehemu mbalimbali kwa ndege ili kuhakikisha kazi ziendeshwe vizuri.

    Kampuni yake ina hekta 80 za mashamba mjini Kunshan, eneo hili ni dogo zaidi kuliko eneo la mashamba lililoko mkoani Hebei ambalo ni hekta 3333 na lile la mji wa Chongqing ambalo ni hekta 11333, lakini Bw. Huang anatilia manani mashamba ya huko, na kuanzisha makao makuu ya kampuni yake mjini Kunshan. Alisema kutokana hali nzuri ya kijiografia ya Kunshan na athari kubwa ya kiuchumi ya mji huo, shughuli zake mjini humo zitakuwa na mustakabali mzuri.

    Licha ya matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji, Bw. Huang pia anatumia mawazo la kisasa katika mauzo ya bidhaa zake. Alisema hivi sasa kampuni yake inajenga tovuti ili kutangaza habari mbalimbali za kampuni yake kupitia Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako