• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yasema mambo ya Asia yanapaswa kutatuliwa na kuamuliwa na Asia

    (GMT+08:00) 2014-04-16 18:09:21

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, mambo ya Asia yanapaswa kutatuliwa na na kuamuliwa na Asia yenyewe. Bi Hua Chunying amesema hayo alipokuwa akizungumzia mkutano wa wakuu kuhusu kukuza ushirikiano na kujenga uaminifu barani Asia utakaofanyika mjini Shanghai. Amesema China, ambayo ni nchi mwenyekiti wa mkutano huo kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2016, inataka kutumia fursa ya mkutano huo kuzihimiza nchi za Asia zijenge mtizamo mpya wa usalama katika bara hilo.

    Habari zinasema, nchi na jumuiya za kimataifa karibu 40 zitatuma wawakilishi wao kwenye mkutano huo, na wakuu wa nchi 14 pamoja na wakurugenzi wanane wa mashirikia ya kimataifa wamethibitisha kuhudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako