• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukraine iko kwenye hatari ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe

    (GMT+08:00) 2014-04-16 19:01:21

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, hali nchini Ukraine inazidi kuwa mbaya, na nchi hiyo iko katika hatari ya kuingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Rais Putin amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel kwa njia ya simu.

    Viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu kitendo cha serikali ya Kiev cha kutumia nguvu kuzuia maandamano katika sehemu ya kusini mashariki mwa Ukraine, ambacho kinaenda kinyume cha katiba ya nchi hiyo. Wamesisitiza umuhimu wa majadiliano kati ya Russia, Umoja wa Ulaya, Marekani na Ukraine yatakayofanyika kesho mjini Geneva na kutarajia majadiliano hayo yatahimiza utatuzi wa amani wa suala hilo.

    Wakati huo huo, rais Putin pia alisisitiza umuhimu wa kulinda utulivu wa kiuchumi wa Ukraine na usalama wa kituo cha kusafirisha gesi kutoka Russia kwenda Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako