• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yaidhinisha makubaliano ya kibiashara kati yake na kenya.

    (GMT+08:00) 2014-04-16 19:23:38

    Kenya- Bunge la Ethiopia limeidhinisha makubaliano yaliotiwa saini kati ya nchi hiyo na kenya ambayo yatawezesha wafanyibiashara wa kenya kuendesha shughuli zao nchini humo.

    Pamoja na mambo mengine makubaliano hayo yatawezesha benki za Kenya kufungua ofisi nchini Ethiopia.

    Na sio tu wakenya watafungua bishara nchini Ethiopia lakini pia wafanyibiashara wa Ethipia wataweza kuendesha shughuli zao nchini kenya chini ya makubalinao hayo mapya.

    Makubalinao hayo yalitiwa saini mwezi Machi wakati Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipozuru Addis Ababa na idhini hiyo ya bunge inatarajiwa kuchapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali ili kuifanya sheria.

    Biashara kati ya Nairobi na Addis Ababa inafaidi sana kenya. Mwaka wa 2012 Kenya iliuza bidhaa za dhamani ya dola milioni 54 nchini Ethipia huku nayo Ethiopia ikiuzia Kenya bidhaa za dola milioni 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako