• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje ya China akutana na kiongozi wa chama cha upinzani cha Syria

    (GMT+08:00) 2014-04-16 20:18:54

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Syria NCSR Bw. Ahmad al-Jarba.

    Bw. Wang Yi amesema, ili kutatua mapema suala la Syria kwa njia ya kisiasa, ni lazima pande mbalimbali nchini Syria zisimamishe haraka mapigano, kuhimiza mchakato wa mpito wa kisiasa, kutekeleza kwa pande zote azimio la No. 2139 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Bw. Wang Yi ameongeza kuwa, China inapenda kuendelea na mazungumzo na pande mbalimbali nchini Syria kikiwemo chama cha Bw. Jarba, na kufanya kazi ya kiujenzi katika utatuzi wa suala la Syria.

    Bw. Jarba amesema, chama chake kinapinga kithabiti ugaidi, na kama serikali ya Syria ina moyo wa dhati, kinapenda kushiriki kwenye duru ya tatu ya mazunguzmo kuhusu suala la Syria itakayofanyika huko Geneva. Pia ameeleza matumaini yake kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo unaokubaliwa na pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako