Mkutano wa kilele wa kuhusu uchumi wa Afrika wajadili njia ya maendeleo ya Afrika Mkutano wa kilele kuhusu Afrika wa Baraza la uchumi wa dunia ulimalizika jana huko Abuja, Nigeria. Katika mkutano huo wa siku 3, wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wapatao 900 kutoka nchi zaidi ya 70 duniani walijadili mada mbalimbali zikiwemo namna ya kupata maendeleo ya haki na usawa, jinsi kuongeza nafasi za ajira na mwelekeo wa uchumi wa Afrika.
Hotuba iliyotolewa na waziri mkuu wa China kwenye Baraza la uchumi la dunia yavutia mwitikio mkubwa Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye alikuwa ziarani nchini Nigeria jana alitoa hotuba kwenye mkutano wa 24 wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia unaofanyika mjini Abuja, akisisitiza kuwa kujitokeza kwa Afrika kunasaidia amani na maendeleo ya dunia, na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika na unahimiza maendeleo yenye uwiano ya uchumi wa dunia wenye ongezeko kubwa linalonufaisha watu kwa haki na usawa. Hotuba yake imevutia mwitikio mkubwa.
Waziri mkuu wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia Nafurahi ujumbe wa serikali ya China ambao si nchi ya Afrika kuhudhuria pamoja nami kwenye mkutano wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi la dunia. Namshukuru Bw. Klaus Schwab kwa kunialika, na namshukuru rais Jonathan kwa mapokezi mazuri. Kauli mbiu ya mkutano huu ni "Kufaidika na ongezeko la uchumi kwa haki na usawa, na kuleta nafasi za ajira", ambayo inaendana na hali halisi na ina mvuto mkubwa.