• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini China yapata maendeleo

    (GMT+08:00) 2014-06-26 18:48:32

    Leo si siku ya 27 ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya. Dawa za kulevya zimekuwa ni tishio jipya kubwa kwa binadamu. Hapa China, tangu mwaka 2005 jamii imehamasishwa kushiriki kwenye mapambano dhidi ya dawa hizo kwa njia moja au nyingine, na mpaka sasa maendeleo yamepatikana katika vita hiyo, upandaji wa mipopi kwa wingi umetokomezwa, hna watu wengi waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wamefanikiwa kuachana na matumizi ya dawa hizo na kurudi kwenye jamii. Fadhili Mpunji anaeleza zaidi:

    Xu Zhiying anayetimiza umri wa miaka 40 alikuwa anatumia dawa za kulevya. Baada ya kutoka kituo cha kuwasaidia watu kuacha matumizi ya dawa za kulevya, amejitajidi kurudi kwenye maisha ya kawaida, huku akijitolea kuwasaidia watumiaji wengine wa dawa hizo kuacha kuzitumia.

    "Kutokana na uzoefu wangu, naona ajira ni muhimu sana kwa mtu kujirudia katika maisha ya kawaida, kama asipokuwa na ajira ni vigumu, sababu mtizamo wake utabadilika, hasa watu waliowahi kutumia dawa za kulevya. Baada ya kutoka kituo cha kusaidia kuacha matumizi ya dawa za kulevya, kitu cha kwanza ni kujipatia ajira. Mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji juhudi za jamii. Sasa nimepata fursa ya kuwasaidia wengine, najaribu kubadilisha mitazamo yao kuhusu maisha."

    Mke wa Xu Zhiying, ambaye anamiliki kampuni, Lin Xiuping anamwunga mkono mume wake kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwapa baadhi yao kazi katika kampuni yake. Na hao watu waliopata kazi wanajitokeza kuwasaidia wengine.

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya kupambana na dawa za kulevya Liu Yuejin amefahamisha kuwa, idadi ya watu wanaojitolea kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya kama walivyo Xuzhiying na mke wake imefikia milioni moja, mbali na hayo, kuna mashirika zaidi ya 700 nchini China yanayofanya kazi ya kupambana na dawa hizo, na vituo zaidi ya 20 vya ngazi ya mkoa ambavyo vinajishughulisha na kuwaelimisha watu kuhusu madhara ya dawa za kulevya. Kutokana na juhudi hizo nchini, kasi ya ongezeko la idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya imepungua hadi asilimia 6.6 ya mwaka 2013 kutoka asilimia 13.7 ya mwaka 2008, na idadi ya watu wasiorudia tabia hiyo miaka mitatu baada ya kuiacha imefikia laki 8.8.

    Hata hivyo, mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini China yanakabiliwa na changamoto nyingi, na mojawapo ni vyanzo vingi vya dawa hizo kuwa nje ya nchi. Kutokana na hali hiyo China imekuwa ikiimarisha ushirikiano wa kimataifa katika eneo hilo. Li Zhuqun ni ofisa kutoka idara ya ushirikiano wa kimataifa katika wizara ya usalama wa umma ya China.

    "kwa upande mmoja, China imesaini mikataba kuhusu ushirikiano katika kupambana na dawa za kulevya na nchi au jumuiya zaidi ya 20, kuanzisha utaratibu wa kufanya mkutano kila mwaka na Marekani, Russia, Laos na Myanmar. Ushirikiano huo hauishii tu kwenye kubadilishana taarifa, umepanuliwa hadi kwenye maeneo ya kubadilishana ushahidi, kufanya mahojiano kwa pamoja na kukabidhiana watuhumiwa. Aidha, China inafanya operesheni kadhaa kila mwaka katika sehemu za mipakani ili kuzuia dawa za kulevya kuingia nchini. Kwa upande mwingine, wizara yetu inajaribu kuongeza bajeti ya misaada kwa nchi jirani zenye vyanzo vya dawa za kulevya au zenye njia za kusafirisha dawa hizo, kwa ajili ya kuimarisha mikakati yao ya kupambana na dawa hizo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako