• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu waanza kufanyika kwa kasi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2014-07-16 09:29:44

    Katibu mtendaji wa Mpango mpya wa wenzi wa maendeleo ya Afrika (NEPAD) Bw. Abdoul Salam Bello hivi karibuni ametoa makala kwenye gazeti la Afrika Vijana akisema, uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu umeanza kufanyika kwa kasi kubwa barani Afrika.

    Mwezi Juni mwaka jana, rais Barack Obama wa Marekani alitoa mpango wa Afrika yenye umeme. Kutokana na mpango huo, Marekani itatoa dola za kimarekani bilioni 7 katika miaka mitano ijayo, ili kuzisaidia nchi za Afrika kuendeleza uzalishaji wa umeme. Mpango huo utatekelezwa kwanza nchini Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania, na kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kwenye nchi hizo, na kunufaisha kampuni na familia milioni 20. Mpango huo wa Marekani pia umeivutia Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na baadhi ya kampuni binafsi za Afrika. Kwa mfano kampuni ya Heirs ya Nigeria imetangaza kutoa dola za kimarekani bilioni 2.5 na kuchangia kwenye mpango huo.

    Hivi sasa kampuni nyingi zaidi za China zinashiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika. Mwaka jana, Kenya na China zilisaini makubaliano ya kupata mkopo wa dola za kimarekani bilioni 5, ambao utatumika kujenga reli moja kutoka Mombasa hadi mpaka wa Uganda, na urefu wa reli hiyo utafikia kilomia 952. Reli hiyo pia inatarajiwa kurefushwa hadi Rwanda, Uganda, na Tanzania ifikapo mwaka 2018.

    Katika miaka kadhaa iliyopita, nchi nyingi za Afrika zilitoa dhamana na kukusanya fedha ili kuwekeza kwenye ujenzi wa miundo mbinu. Mwaka 2012, nchi za Afrika zilitoa dhamana ya dola za kimarekani bilioni 8.1 kwa jumla. Hivi karibuni, Kenya imekusanya dola za kimarekani bilioni 25 kupitia njia ya kutoa dhamana ya nchi, ili kuwekeza kwenye ujenzi wa bandari ya pili ya nchi hiyo, bomba moja la kusafirisha mafuta, na barabara moja itakayofungua soko la usafirishaji nje ya Afrika Mashariki.

    Njia nyingi muhimu za kukusanya fedha ni mapato ya fedha za kigeni zinazotumwa na waafrika kwenye nchi zao. Mapato ya fedha hizo barani Afrika mwaka 2012 yalikaribia dola za kimarekani bilioni 40, na kuzidi thamani ya jumla ya msaada wa maendeleo inayopata Afrika kila mwaka. Nchi za Afrika zinaweza kutumia vizuri mapato ya fedha zinazotumwa na waafrika kwa nchi zao, kwa mfano, katika miaka kadhaa iliyopita, Ethiopia ilitoa dhamana mara mbili kwa waethiopia wanaoishi katika nchi nyingine, moja ni kuwekeza kwenye kampuni ya uzalishaji wa umeme ya Ethiopia, na nyingine ni kuwekeza kwenye mradi wa uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji nchini humo.

    Mwezi Julai mwaka jana, Benki ya Maendeleo ya Afrika ilizindua Mfuko wa Afrika katika miaka 50 ijayo, na kuwekeza ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika. Benki ya Dunia pia inafanya juhudi za kuanzisha mfumo wa uwekezaji wa dunia, ambao utatoa huduma mfululizo, na kuunganisha ukusanyaji wa fedha na uwekezaji wa miradi.

    Lakini Bw. Abdoul Salam Bello pia alisema, ingawa kuna njia nyingi za kukusanya fedha, lakini bado kuna upungufu wa fedha za ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika. Kwa upande mmoja, mazingira ya sheria na utaratibu wa baadhi ya nchi za Afrika bado vinahitaji kuboreshwa zaidi, na kwa upande mwingine, nchi za Afrika hazina uzoefu wa kutosha katika kukusanya fedha.

    Bw. Abdoul Salam Bello amesema, kampuni binafsi zinaweza kutoa mchango kwa kutatua suala la upungufu wa fedha za ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika. Katika siku za baadaye, nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha imani ya uwekezaji wa kampuni binafsi, kupunguza hatari yao ya uwekezaji, na kulinda maslahi ya wawekezaji kwa kupitia mfumo wa sheria na utaratibu.

     

    China na Marekani zafikia makubaliano 300 ya ushirikiano kwenye mazungumzo kati yao kuhusu mkakati na uchumi

    Mazungumzo ya duru ya sita kati ya China na Marekani kuhusu mkakati na uchumi yamefanyika hivi karibuni hapa Beijing, ambapo nchi hizo mbili zimefikia makubaliano karibu 300 ya ushirikiano kwenye mambo ya mkakati, uchumi, utamaduni na jamii. Makubaliano hayo yamefikiwa na idara nyingi za China na Marekani katika kipindi cha mazungumzo ya duru ya sita kati ya nchi hizo mbili kuhusu mkakati na uchumi, na mazungumzo ya duru ya tano kati yao kuhusu mawasiliano ya utamaduni na jamii.

    Orodha ya mafanikio ya mazungumzo kati ya China na Marekani kuhusu mkakati inaonesha kuwa, viongozi wa nchi hizo mbili wataendelea kudumisha mawasiliano mara kwa mara kwa kupitia ziara, mikutano, simu, na barua. Pande hizo mbili zilizoshiriki kwenye mazungumzo hayo zimesema zitafanya maandalizi ya mkutano wa viongozi wao utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu mjini Shanghai. Nchi hizo pia zimekubali kufanya ushirikiano kati yao kwenye kupambana na ugaidi, utekelezaji wa sheria, kupambana na ufisadi, forodha, uvuvi na mambo ya bahari, nishati, mabadiliko ya hali ya hewa, na usalama.

    China na Marekani zimefikia makubaliano zaidi ya 90 kwenye mazungumzo ya uchumi, ambayo ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa sera za uchumi, kuhimiza biashara na uwekezaji wa wazi, kuinua kanuni za kimataifa za ushirikiano, na kuunga mkono utulivu wa fedha na mageuzi. Kwenye mazungumzo hayo, China na Marekani pia zimethibitisha ajenda ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati yao, BIT. Zimekubali kufikia maoni ya pamoja kuhusu masuala makuu ya mswada wa BIT mwaka 2014, pia zimeahidi kuanza mazungumzo mapema mwaka 2015 kuhusu mambo yenye migongano. Suala hili limesifiwa na naibu waziri wa fedha wa China Bw. Zhu Guangyao kuwa ni maendeleo ya kihistoria.

    Marekani inazikaribisha kampuni za China kuwekeza nchini humo, na imeahidi kudumisha mazingira ya uwekezaji ya wazi kwa wawekezaji wa aina mbalimbali, na imeahidi kuwa miradi ya uwekezaji kutoka nchi nyingine inayokaguliwa na kamati ya uwekezaji wa nje ya Marekani itatumia kanuni na vigezo za pamoja. Pia nchi hiyo imeahdi kuendelea na majadiliano na mawasiliano na upande wa China kuhusu utaratibu wa ukaguzi kwa wawekezaji wa nchi nyingine, na imeahidi kuipa China hadhi ya usawa katika mchakato wa mageuzi ya usimamizi na udhibiti wa usafirishaji kwa nje. China na Marekani pia zimefikia makubaliano ya kiserikali kuhusu sheria ya kodi ya akaunti ya nje, ili kupambana na vitendo vya kuepusha kodi. Marekani imeahidi kuyachukulia mashirika ya fedha ya China kuwa ya haki. Nchi hizo mbili pia zimetangaza kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata udhamini wa masomo kati yao, vilevile zitaimarisha mawasiliano kati ya majumba ya makumbusho, makundi ya sanaa, na mashirika ya utafiti na taaluma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako