• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  uliokithiri utotoni linazidi kuwa tatizo la afya duniani

    (GMT+08:00) 2014-07-16 16:39:25
    Uzito wa kupindukia miongoni mwa watoto linakuwa tatizo la afya ya umma katika nchi nyingi zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. WHO inasema idadi ya watoto wenye unene wa kupindukia kote duniani imeongezeka kutoka milioni 31 mwaka 1990 hadi milioni 44 wakati huu, huku nchi zinazoendelea zikishuhudia kiwango cha ongezeko kilicho asilimia 30 zaidi ya kile cha nchi zilizoendelea. Barani Afrika, takriban watoto milioni 10 wanaainishwa kama wenye uzito uliokithiri. Ilikukabiliana na tatizo hili sugu la unene uliokithiri miongoni mwa watoto, wiki hii WHO inafanya mkutano wa kwanza kabisa wa Kamisheni ya Kutokomeza Uzito Uliokithiri Utotoni. "Kamisheni hii itachuguza hali zote zinazochangia unene wa kupindukia wa watoto wadogo. Hatua ya WHO ni kufuata mpango mathubuti wa kimataifa kuhusu mlo, mazoezi ya kimwili kwa ngazi za kimataifa, kikanda na hata mitaani. Sehemu ya hatua hiyo ni kamisheni hii- inaangazia kila kinachohusiana na unene uliokithiri, kuanzia utangazaji wa vyakula vya watoto wachanga, njia za kuuzuia unene huo, kuupunguza katika watoto walioathiriwa tayari, na sera bora zinazoweza kuwekwa ili kuyafikia malengo haya” Dan Epstein wa WHO anaeleza. WHO imesema watoto walio na uzito wa kupindukia wamo hatarini zaidi kubaki na uzito uliokithiri hata wakiwa wakubwa, na kupata magonjwa yasiyo ya kuambukizakamavile kisukari na magonjwa ya moyo katika umri mdodgo. Ili kukabiliana na uzito uliokithiri, WHO inapendekeza mazoezi ya mwili mara kwa mara, kula matunda na mboga za majani zaidi, vitu kamamaharage, bidhaa za nafaka, na kupunguza matumizi ya mafuta na sukari.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako