• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UN anaamini mapambano ya Gaza yataisha karibuni

    (GMT+08:00) 2014-07-23 10:25:33

    Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki Moon amesema anaamini kuwa mazungumzo aliyofanya na viongozi mbalimbali duniani yatasaidia kukomesha mapambano kati ya Israel na kundi la Hamas katika siku za hivi karibuni. Bw Ban Ki Moon alisema hayo baada ya kuliarifu baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu hali ya Gaza.

    Habari kutoka Ramallah, Palestina zinasema hadi sasa idadi ya watu waliouawa imefikia 631, kati yao kuna watoto 161, wanawake 66 na wazee 55, na kwa upande wa Israel, raia mmoja wa Israel na wanajeshi 25 wameuawa na mwanajeshi mmoja alitekwa nyara na kundi la Hamas.

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw Liu Jieyi amezitaka Israel na Palestina kusimamisha mapambano na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kufikia makubaliano ya kusimamisha vita bila masharti. Na mjumbe wa China anayeshughulikia suala la mashariki ya Kati Bw Wu Sike amesema anaunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na Misri kuhusu kusimamisha mapambano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako