• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa 229 wa ngazi ya mikoa nchini China waamriwa kuachia nafasi walizo nazo kwenye makampuni

    (GMT+08:00) 2014-07-23 19:08:03

    Takwimu zilizotolewa leo na serikali ya China zinaonyesha kuwa, jumla ya maofisa 229 wa ngazi za mikoa na wizara wameamriwa kujiuzulu nafasi walizo nazo kwenye makampuni mbalimbali kwa lengo la kuondoa mgongano wa maslahi unaotokana na mpangilio huo. Tayari maofisa 173 wametekeleza agizo hilo, na wengine wamewasilisha barua za kujiuzulu nyadhifa zao, lakini bado wanaendelea na nyadhifa zao mpaka warithi wao watakapopatikana.

    Mwezi Oktoba mwaka jana, idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ilitoa waraka unaowazuia maofisa wa serikali na Chama kufanya kazi kwenye makampuni ya nje. Idara hiyo imesema, kutokana na waraka huo, ukaguzi maalum umefanyika na maofisa zaidi ya elfu 40, wakiwemo 229 wa ngazi ya mikoa na wizara, wamekutwa wakiwa na nafasi nyingine kama wakurugenzi au wasimamizi katika makampuni binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako