Wanawake nchini Saudi Arabia wataruhusiwa kugombea na kupiga kura katika uchaguzi wa mabaraza ya manispaa utakaofanyika mwaka ujao. Awali, wanawake hawakuruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2011, lakini mara baada ya uchaguzi huo, mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al Saudi Bunge la nchi hiyo alitoa amri ya kuwaruhusu wanawake kushiriki kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani na chaguzi zitakazofuata.
Wagombea wote wa kike na wa kiume hawatakiwi kuwasilisha picha zao ili kutowalazimisha wanawake kuonesha sura zao, kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili ya jamii ya Saudi Arabia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |