• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara ya huduma yatoa msukumo mpya kwa biashara ya China nchi za nje

    (GMT+08:00) 2014-07-23 19:25:24

    Wizara ya biashara ya China imesema, biashara ya huduma imetoa msukumo mpya kwa biashara ya China nchi za nje ambayo inadidimia.

    Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara ya huduma ya China ilifikia dola bilioni 285 za kimarekani. Inakadiriwa kuwa, katika siku za baadaye kasi ya ongezeko la biashara ya huduma itazidi ile ya biashara ya bidhaa, na itakapofika mwaka 2020, thamani yake itazidi dola trilioni 1.2 za kimarekani.

    Biashara ya huduma pia imesaidia wahitimu wa vyuo vikuu kupata ajira. Tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2011, wanafunzi karibu milioni 6 waliohitimu vyuo vikuu walipata ajira kutokana na biashara ya huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako