• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani awasili Israel kwa ajili ya kuhimiza kusimamisha mapigano katika ukanda wa Gaza

    (GMT+08:00) 2014-07-23 20:08:56

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. John Kerry amewasili Israel kwa ajili ya upatanishi kati ya Israel na Hamas ili zifikie makubaliano ya kusimamisha mapigano.

    Ubalozi wa Marekani huko Tel Aviv umesema, Kerry aliyetokea Cairo ambako alikutana na maofisa wa Misri, leo anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, rasi wa Palestina Mahmoud Abbas, na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko kwenye kanda hiyo ikiwa ni juhudi za kidiplomasia za kusimamisha mapigano kwenye ukanda huo.

    Maofisa wa afya wa Gaza wamesema, tangu operesheni ya kijeshi ya Israel ianze Julai 8, wapalestina zaidi ya 600 wakiwemo wanawake, watoto, wazee, na watu wasiojiweza, wameuawa na wengine zaidi ya 3,000 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel.

    Habari nyingine zinasema, askari 29 wa Israel wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa tangu operesheni ya ardhini ianze katika ukanda wa Gaza. Raia wawili wa Israel waliuawa wiki iliyopita wakati kundi la Hamas liliporusha makombora zaidi ya 2,000 katika sehemu mbalimbali kusini mwa Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako