• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge wa Somalia auawa mjini Mogadishu

    (GMT+08:00) 2014-07-23 21:05:36

    Mbunge mmoja wa kike wa Somalia ameuawa leo mjini Mogadishu na watu wenye silaha. Mbunge huyo Saado Ali Warsame ambaye pia ni mwimbaji mashuhuri nchini humo aliuawa akiwa ndani ya gari lake alipokuwa akielekea hoteli kwake.

    Warsame ni mbunge wa nne kuuawa mwaka huu katika mashambulizi ambayo yanazidi kuwalenga wabunge wa bunge la nchi hiyo. Dereva wa Warsame pia ameuawa katika shambulizi hilo lililotokea katika mtaa wa Hodan mjini humo, ambao ulidhaniwa ni mtaa salama zaidi kutokana na uwepo wa wanausalama wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako