• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Palestina na Israel zinapaswa kusimamisha vita mara moja

    (GMT+08:00) 2014-07-28 17:45:41

    Mgogoro kati ya Palestina na Israel ambao umedumu kwa zaidi ya siku 20, hadi sasa umesababisha vifo vya watu wasiopungua 1000 na wengine zaidi ya 6000 kujeruhiwa. Mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Mashariki ya Kati Bw. Wu Sike, amesema kusimamisha vita ni jambo la dharura kwa Palestina na Israel, na hiyo ni njia pekee ya kuepusha vifo na majeruhi ya watu. Hivi karibuni Bw. Wu alifanya ziara katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati kufanya juhudi za kusuluhisha mgogoro huo. 

    Ili kuondoa hali ya wasiwasi ya kanda ya Mashariki ya Kati iliyosababishwa na mgogoro kati ya Palestina na Israel na mgogoro nchini Iraq, mwezi huu Bw. Wu Sike amefanya ziara mbili za usuluhishi katika kanda ya Mashariki ya Kati. Kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 26 Julai, Bw. Wu alitembelea Israel, Palestina, Jordan, Misri, Qatar na makao makuu ya Umoja wa nchi za Kiarabu, kukutana na viongozi wa nchi husika, na kuzihimiza pande mbili kufanya juhudi pamoja ili kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel. Bw. Wu Sike amesema China inafuatilia kwa karibu hali ya ukanda wa Gaza, na inasikitishwa na kupamba moto kwa mgogoro wa kijeshi na vifo na majeruhi ya watu wengi,

    "Kusimamisha vita ni jambo la dharura. China, Israel na Palestina zote zinasisitiza jambo hili. Jumuiya ya kimataifa imetoa wito kuzitaka Israel na Palestina kusimamisha vita ili kuepusha vifo na majeruhi ya raia wa kawaida."

    Tarehe 14 wizara ya mambo ya nje ya Misri ilitoa taarifa ikizihimiza Palestina na Israel kusimamisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, na kuhakikisha watu na vitu vinaingia katika ukanda wa Gaza kwa usalama. Taarifa hiyo pia inapendekeza pande mbili zifanye mazungumzo na Misri mjini Cairo. Bw. Wu Sike amesema China inaunga mkono mapendekezo ya Misri, na inaona mapendekezo hayo yameweka msingi mzuri wa kutatua kabisa suala la Palestina. Amesisitiza kuwa kurejesha mazungumzo ya amani, na ni jambo muhimu katika kutatua suala la Palestina.

    "Ukweli wa mambo umethibitisha kuwa usalama hautaweza kupatikana kwa nguvu za kijeshi, bali unaweza kupatikana kwa njia ya mazungumzo. Hivyo nilipowasiliana na pande mbili, ninasisitiza maoni ya China kuwa hatua za kijeshi hazisaidii kutatua matatizo, isipokuwa zinavuruga amani."

    Bw. Wu Sike pia amesema tangu mgogoro wa ukanda wa Gaza uzuke, licha ya kutumwa kufanya usuluhishi, serikali ya China pia imewasiliana na pande husika kwa njia mbalimbali,

    "Naibu waziri wa mambo ya nje wa China na viongozi wa idara ya Asia na Afrika ya wizara hiyo wamekutana na mabalozi wa Israel, Palestina na baadhi ya nchi za Kiarabu na wajumbe wa Umoja wa nchi za Kiarabu, kuzishauri pande mbili za mgogoro kurejesha mazungumzo. Wasemaji wa wizara ya mambo ya nje wameeleza msimamo wa China kuhusu hali ya Palestina na Israel mara kwa mara, na wajumbe wa China katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine pia wametoa maoni ya haki na usawa kuhusu suala hilo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako