• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nafasi za ajira zaongezeka wakati kasi ya ongezeko la uchumi inapopungua nchini China

    (GMT+08:00) 2014-07-30 09:51:30

    Hivi sasa kasi ya ongezeko la uchumi wa China imepungua, lakini katika mazingira hayo, mwelekeo wa kuongezeka kwa nafasi za ajira umetokea. Wachambuzi wanaona kuwa hali hiyo inaambatana na mchakato wa mabadiliko ya muundo wa uchumi, pia itahimiza mabadiliko hayo.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang hivi karibuni amesema, kama China ikiweza kuhakikisha utoaji wa nafasi za ajira, kuongeza kipato cha raia, kuinua sifa na ufanisi, kuhifadhi mazingira, na kupunguza matumizi ya nishati, ni wazi kuwa kasi ya ongezeko la uchumi wa China itapungua kuliko asilimia 7.5 kwa kiasi kidogo au kuzidi asilimia 7.5.

    Wachambuzi wanaona kuwa, kutoa kipaumbeke kwa upatikanaji wa nafasi za ajira katika maendeleo ya uchumi, ni hatua muhimu kwa China kupunguza kasi ya ongezeko la uchumi, kutilia maanani ongezeko la utulivu, kurekebisha muundo wa uchumi, kuhimiza mageuzi, na kunufaisha maisha ya raia, pia wanaona hatua hiyo itahimiza marekebisho ya muundo wa uchumi.

    Profesa wa Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Lu Feng amesema, ongezeko la nafasi za ajira na marekebisho ya muundo wa uchumi ni pande mbili za suala moja, ambazo zitatokea kwa wakati mmoja katika mchakato wa utandawazi wa miji na viwanda.

    Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na idara ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, ongezeko la uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu limefikia asilimia 7.4, na kukaribia lengo la asilimia 7.5 lililowekwa mwanzoni mwa mwaka huu. Wakati huo huo, idadi ya watu waliopata nafasi za ajira katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imezidi milioni 7, na lengo lililowekwa mwanzoni mwa mwaka huu ni watu milioni 10.

    Lengo la ongezeko la uchumi wa China lililowekwa hapo awali limezingatia mahitaji na uwezekano, lengo la kuhakikisha ongezeko la utulivu ni kuhakikisha utoaji wa nafasi za ajira, hii si kama tu inatakiwa kukidhi mahitaji ya kuongezeka kwa nafasi mpya za ajira mijini, bali pia inatakiwa kutoa nfasi za ajira kwa wakulima waliokwenda mijini kutoka vijijini.

    Kuhusu uhusiano kati ya ongezeko la uchumi na nafasi za ajira, naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti ya kituo cha kimataifa cha mawasiliano ya uchumi cha China Bw. Wang Jun amesema, kama ongezeko la uchumi wa China halitapungua sana na kuathiri vibaya nafasi za ajira, hakuna haja ya kuzingatia mabadiliko madogo ya kasi ya ongezeko hilo, na China inapaswa kutilia maanani kurekebisha muundo wa uchumi na kuhimiza mageuzi.

    Tangu msukosuko wa fedha kutokea duniani, kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2013, ongezeko la uchumi wa China limepungua hatua kwa hatua kutoka aslimia 10.3 hadi aslimia 9.2, asilimia 7.8 na asilimia 7.7. Lakini wakati huo huo, idadi ya watu waliopata ajira mijini imeongezeka kutoka milioni 11.68 hadi milioni 12.21, milioni 12.66 na milioni 13.10, ambapo imeongezeka kwa miaka minne mfululizo. Uchumi wa China unabadilika kuwa uchumi unaoongozwa na sekta ya huduma, kutoka uchumi ulioongozwa na sekta ya viwanda. Sekta ya huduma ina mahitaji makubwa kwa nafasi za ajira.

    Licha ya kuhinmiza ongezeko la idadi ya nafasi za ajira kutokana na marekebisho ya muundo wa uchumi, wachambuzi pia wanaona kuwa, serikali inafanya juhudi kuhakikisha maisha ya raia, na kulinda mstari wa mwisho wa nafasi za ajira, pia ni sababu nyingine ya ongezeko la nafasi za ajira.

    Lakini wachambuzi pia wamesema, ingawa idadi ya watu waliopata nafasi za ajira inaongezeka nchini China, lakini kwa mfanyakazi binafsi, lazima kuongeza uwezo na ufundi wake, ili kuambatana na matakwa ya soko.

    Wataalamu wakusanyika huko Kashi na kutoa mapendekezo kwa ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya hariri

    Mkutano wa kwanza wa Baraza la kimataifa la eneo la uchumi la Njia ya hariri umefanyika huko Kashi, Xinjiang, nchini China na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi za eneo la uchumi la Njia ya hariri, pamoja na Thomas Sargent aliyepewa tuzo ya Nobel ya uchumi mwaka 2011, na maofisa wa kampuni kubwa 500 duniani. Wajumbe hao wametoa mapendekezo kwa ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya hariri.

    Mkutano huo umefuatilia ushirikiano wa kikanda kati ya sehemu ya Asia Kati, ambao ni pamoja na ushirikiano wa kifedha, maendeleo ya mambo ya utamdaduni na utalii, kujenga kituo muhimu cha mawasiliano cha Njia ya hariri ya anga, kuhimiza nguvu ya uhai wa utengenezaji, na maendeleo ya sekta mpya na nishati mpya.

    Thomas Sargent amesema, eneo la uchumi la Njia ya hariri lilitolewa kwa makini, na litaimarisha hadhi ya kimkakati na kuhimiza maendeleo ya Kashi, vilevile litaongoza mawasiliano ya uchumi na utamaduni wa nchi za eneo la uchumi la Njia ya hariri, hivyo litahimiza maendeleo ya uchumi wa kikanda, na kusaidia kutuliza hali ya Asia ya Kati.

    Balozi wa Azerbaijan nchini China anakubaliana na maoni ya Bw. Sargent, na kuongeza kuwa, nchi mbalimbali za eneo la uchumi la Njia ya hariri zina maliasili nyingi zenye umaalumu, na raslimali za utamaduni na historia. Kujenga eneo la uchumi la Njia ya hariri si kama tu kutaendeleza nchi moja, bali ni kuhimiza maendeleo ya kanda na nchi mbalimbali za eneo hilo zitanufaika kutokana na ujenzi huo.

    Balozi huyo amesema, kuhimiza ujenzi wa eneo la uchumi la Njia ya hariri lazima kuendane na maendeleo ya mawasiliano na usafirishaji. Amesema China na Azerbaijan ni nchi jirani sana, ambazo utamaduni wao unafanana, hivyo ana imani kubwa Njia ya hariri itaimarisha uhusiano na mawasiliano kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. David Schlesinger ambaye aliwahi kuwa mhariri mkuu wa shirika la habari la Reuters ameona kuwa, hivi sasa nchi za eneo la uchumi la Njia ya hariri zinatakiwa kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu zikiwemo barabara na bandari. Wakati huo huo, ameona kuwa ni muhimu sana kuinua kiwango cha maisha na elimu ya wakazi wa huko.

    Bw. Schlesinger aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu nchini China, hivyo amezoea hali ya China, na kusema China inapaswa kutoa mchango katika kulinda utulivu wa kikanda kama China na mkoa wa Xinjiang zinataka kupata maendeleo.

    Mjumbe mkuu wa China kwenye mazungumzo kuhusu kujiunga na shirika la biashara duniani IMF Bw. Long Yongtu amesema, ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda unasaidia kuhimiza amani na utulivu wa kanda hiyo, kuhimiza mawasiliano ya uchumi, na kuhimiza usawa wa maendeleo ya nchi mbalimbali za kanda hiyo. Amesema, ikiwa mji muhimu wa eneo la uchumi la Njia ya hariri, mji wa Kashi unaweza kujaribu kutekeleza sera zinazotoa urahisi ili kuhimiza biashara na uwekezaji huria, ni lazima kufanya juhudi na kuendeleza mambo ya huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako