• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Kenya Daniel Moi autilia shaka mpango wa Rais wa Marekani Obama wa vongozi vijana barani Afrika

    (GMT+08:00) 2014-07-31 10:51:13

    Rais wa zamani wa Kenya Daniel Moi amehoji mpango wa Rais wa Marekani wa Young African Leaders Initiative. Julai 29, Moi alikiri kufuatilia kwa makini mpango huo ulioanzishwa na Obama na kugundua kuna maswali mengi yanayotilia shaka nia ya mpango huo.

    Rais huyo wa zamani alidadisi vigezo vya uteuzi wa vijana katika mpango huo, ushirikishi wake na ni nini hasa wanachofundishwa vijana.Alisema wakenya wanafaa kufafanuliwa kwa uwazi utaratibu wa kuwachagua vijana, mtaala wa mafunzo na jinsi vijana hao wanavyolenga kuchukua nafasi za uongozi.

    Moi aliuliza ni wapi viongozi hao vijana walichaguliwa, aliyewachagua na aina ya mafunzo wanayopewa.

    Kauli hiyo ya rais mstaafu inakuja siku moja tu baada ya Barack Obama kukutana na vijana 500 wa Afrika ambao walikuwa wakifunzwa nchini Marekani chini ya mpango wa Young African leadership Initiative. Miongoni mwa vijana hao walikuwa wakenya 47.

    Huku akisema mpango huo umezua maswali mengi kuliko majibu, Moi alikariri kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia ambapo viongozi huchaguliwa kwa kupata kura nyingi, na kuhoji ni jinsi gani vijana hao watakavyochukua nafasi za uongozi.

    Alisema wakenya lazima watilie shaka baadhi ya mipango ambayo huonekana kutokuwa hatari ilhali nia za mipango hiyo inaweza kwenda kinyumea na matakwa ya watu. Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, mpango huo unalenga kubadili fikira za vijana kote barani Afrika. Mpango wa Washington Fellowship for Young African Leaders ambapo wakenya 47 wanashiriki, jana ulibadilishwa jina na kuitwa Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders.

    Tangazo hilo lilitolewa na Rais wa Marekani Barack Obama wakati akihutubia vijana 500 ambao walikuwa wakifunzwa nchini Marekani chini ya mpango wa Young African Leaders Initiative.

    Obama alisema kuwa mpango huo unaashiria baadhi ya maadili ambayo Mandela alikuwa nayo na baada ya kujadiliana na familia yake waliamua kubadili jina la ushirika huo.

    Obama pia alitangaza kuwa vituo vinne vya kikanda vitaanzishwa barani Afrika katika nchi za Kenya, Ghana, Afrika Kusini na Senegal. Alisema vituo hivyo vitahimiza zaidi shughuli za viongozi vijana kutoka mashirika mbalimbali na maeneo tofauti.

    Aliongeza kuwa vituo hivyo vitatoa mafunzo ya hali ya juu ya uongozi, msaada wa ujasiriamali na kuongeza mitandao ya kitaalamu.

    Kituo cha Kenya kitatoa mafunzo ya mtalaa wa mafunzo imara na mwongozo kutokana na ushirikiano ambao utaleta pamoja ujuzi wa kimataifa wa mkakati na usimamizi wa shirika la Deloitte, mtaala imara na uwezo wa chuo kikuu cha Kenyatta, mafunzo ya utawala wa umma kutoka Kenya School of Government na chuo kikuu cha Africa Nazarene.

    Obama alisema kuna haja ya kuanzisha ushirika uliozinduliwa mwaka 2010 ili kuzipanua akili za vijana barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako