• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia yasema uamuzi wa Marekani kuweka vikwazo dhidi ya Russia utatatiza zaidi uhusiano kati yao

    (GMT+08:00) 2014-07-31 11:20:38

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema uamuzi wa Marekani kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Russia kutatatiza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kusababisha athari mbaya kwa ushirikiano kati yao kuhusu mambo ya kimataifa.

    Wizara hiyo pia imesema vikwazo vipya vya Umoja ya Ulaya ya dhidi ya Russia vinaonesha kuwa Umoja huo hauna nia ya kisiasa ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine, na vimekiuka kanuni za Shirika la Biashara Duniani WTO, na vitakuwa na madhara kwa benki za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zilizoko nchini Russia.

    Wakati huohuo, viongozi wa kundi la nchi 7 wametoa taarifa ya pamoja kuionya Russia kuwa kama isipochukua hatua za kutuliza hali ya Ukraine, kundi hilo litaongeza vikwazo na kuifanya Russia ipate hasara kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako