• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema uchumi wa China utakua kwa asilimia 7.5 mwaka 2014

    (GMT+08:00) 2014-07-31 16:14:31

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema, uchumi wa China unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.5 mwaka huu, na gharama ya maisha inakuwa chini ya asilimia 3.

    Shirika hilo limesema, licha ya kupungua kwa uwekezaji na uwezekano wa mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa ununuzi wa nyumba, hatua zilizochukuliwa na serikali kuunga mkono ukuaji zinatarajiwa kufikisha ukuaji huo kwenye lengo la mwaka ambalo ni asilimia 7.5.

    Wakurugenzi wakuu wa Shirika hilo wamekubali kuwa, matarajio ya ukuaji wa China yanahatarishwa na kupungua kwa ufanisi katika uwekezaji, kuongezeka kwa deni la taifa, ukosefu wa uwiano wa kipato, na gharama za kimazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako