• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufanya zoezi la kijeshi pamoja na Marekani na Australia

    (GMT+08:00) 2014-07-31 18:25:15

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Geng Yansheng leo hapa Beijing amesema, China, Marekani, na Australia zitafanya zoezi la pamoja la kijeshi mwezi wa Oktoba mwaka huu.

    Bw. Geng amesema, naibu mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Jenerali Fan Changlong alifanya ziara nchini Australia kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, na kutangaza kuwa, China, Australia, na Marekani zitafanya zoezi la pamoja la jeshi la ardhini. Hatua itakayofuata ni kwa pande hizo tatu kujadiliana maandalizi husika ya zoezi hilo.

    Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hizo tatu kufanya zoezi la pamoja la kijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako