• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki zashirikiana na kampuni za mawasiliano ya simu

    (GMT+08:00) 2014-07-31 19:29:12
    Huku mpambano kwa ajili ya wateja kati ya mabenki na kampuni za mawasiliano ya simu ukiendelea kukua kila uchao,mabenki yamebaini kuwa njia pekee ya kupunguza shinikizo na pia kubaki kuwa mshindani ni kufanya kazi pamoja na kampuni za masiliano. Hatua hii imepelekea idadi ya mabenki kushirikisha shughuli zao za benki za simu ya mkononi na majukwaa ya makampuni ya mawasiliano ya huduma za pesa kwenye simu. Waangalizi wa mambo ya soko nchini Rwanda wanasema kwamba tangazo la hivi karibuni la benki ya KCB Rwanda kuwa limeshirikisha jukwaa lake benki kupitia simu za mkononi na kampuni ya mawasiliano ya MTN na jukwaa la pesa kwenye simu la Tigo ni ishara tosha kwamba ni mkakati wa benki hiyo ili ibaki kwenye ushindani. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Rwanda Maurice Toroitich amesema kuwa hatua hiyo itawezesha wateja wa makampuni ya simu kufikia akaunti zao katika jukwaa moja,na kuwaruhusu kutuma pesa kutoka akaunti zao za benki hadi kwenye simu na pia kutoka kwa simu hadi kwa akaunti zao za benki. Hivi sasa zaidi ya wateja milioni 3.4 wamejiandikisha katika majukwaa matatu ya pesa kwenye simu ya MTN Mobile money,Tigo cash na Airtel money.Benki zinataka kufaidi na majukwaa haya kwa kuanzisha bidhaa mpya,kuongeza amana na kuongeza idadi ya wateja wao.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako