Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Qin Gang leo hapa Beijing amesema, bila ya kujali sababu yoyote, kitendo cha kutumia nguvu kushambulia zana za Umoja wa Mataifa na kusababisha vifo na majeruhi ya raia hakikubaliki.
Bw. Qin Gang amesema, hivi karibuni shule za Umoja wa Mataifa zilizoko kaskazini mwa Gaza zilishambuliwa, China inasikitika na kulaani vikali kitendo hicho. Amesema China inazitaka Israel na Palestina ziitikia mwito wa jumuiya ya kimataifa kusimamisha vita mara moja bila sharti lolote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |