• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa umwagiliaji wayasaidia maeneo yenye ukame kaskazini magharibi mwa China kuongeza uzalishaji

    (GMT+08:00) 2014-08-10 17:57:53

    Mboga mbalimbali zinakua vizuri katika majira ya joto katika mkoa wa Ningxia ulioko kaskazini magharibi mwa China, na hazikabiliwi tena na ukosefu wa maji. Hali hii nzuri inatokana na teknolojia ya umwagiliaji unaobana matumizi ya maji. Teknolojia hii imeanza kutumiwa katika baadhi ya mashamba yenye ukame kaskazini magharibi mwa China, imebadili njia ya jadi ya matumizi ya maji, na kuinua ufanisi wa uzalishaji.

    Mwanakijiji wa kijiji cha Lanxing cha mji wa Yinchuan Bw. Ma Guangjie anasema, ametumia teknolojia mpya ya umwagiliaji kwenye hekta 87 za mashamba yake. Uzalishaji wa nyanya ni tani 1,57.5 kwa hekta, lakini matumizi ya maji ni mita 1,050 za mraba. Maji yanamwagiliwa kwa matone kwenye mizizi ya mimea, na mbolea inawekwa moja kwa moja kwenye maji hayo. Bw. Ma anasema, mwaka 2012 alianza kushughulikia kilimo cha nyanya, bilinganya na pilipili. Mwanzoni alimwagilia maji kwa wingi, na hakumwangilia kwa wakati mara kwa mara. Alitumia mita 3000 za mraba za maji, lakini uzalishaji wa nyanya ulikuwa tani 120 tu kwa hekta.

    Mwaka jana, idara ya mambo ya maji ya kaunti yake ilianza kutoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji kwa matone, ambayo si kama tu inasaidia kubana matumizi ya maji, bali pia inawasaidia wakulima kumwagilia kwa wakati. Bw. Ma anasema, mboga zinahitaji maji katika majira ya joto, sasa teknolojia hii mpya imetatua tatizo la ukosefu wa maji, na kuzifanya nyanya ziwe kubwa na nyekundu. Pia alifahamisha kuwa, nyanya zinazozalishwa kwa kilimo cha kawaida cha kumwagilia maji kwa wingi zinavunwa mwezi Agosti, na zinauzwa yuan moja kwa kilo, lakini nyanya zinazozalishwa kwa teknolojia mpya zinavunwa mwezi Septemba, wakati huo bei itakuwa yuan nne kwa kilo kwa sababu mahitaji ni makubwa sokoni. Teknolojia hii ya umwagiliaji si kama tu imeenezwa kaskazini mwa mkoa wa Ningxia, bali pia imehakikisha ongezeko la uzalishaji na mapato ya wakulima katika sehemu za milimani zilizoko katikati, na kusini mwa mkoa huo.

    Naibu mkuu wa idara ya mambo ya maji ya kaunti ya Tongxin ya mji wa Wuzhong Bw. Yang Zhengwu anasema, wakulima, kwa kutumia teknolojia hii, wameanza kushughulikia kilimo cha mazao ya kiuchumi na kuondokana na umaskini. Zamani wakulima waliweza kupanda mahindi tu kutokana na ukame, lakini sasa hata wanaweza kupanda wolfberry ambayo inahitaji maji mengi. Zamani hekta moja ya shamba la wolfberry ilihitaji mita 9,000 za mraba za maji, baada ya kutumia teknolojia mpya, inahitaji mita 1,800 za mraba tu. Wakulima wakikodisha mashamba yao kwa makampuni, watafanya kazi kwa makampuni hayo na kupata yuan 80 kwa siku. Mapato yao yamehakikishwa.

    Hadi sasa, hekta elfu 110 za mashamba yanatumia teknolojia ya umwagiliaji unaobana matumizi ya maji, na kutimiza ongezeko la uzalishaji kwa asilimia 30, na ongezeko la mapato ya yuan elfu 15 kwa hekta. Eneo la mashamba yanayotumia teknolojia hii pia limeongezeka mikoani Xinjiang na Shaanxi. Hadi mwishoni mwa mwaka jana, eneo la mashamba yanayotumia teknolojia hii mkoani Xinjiang lilizidi hekta milioni 2.3, matumizi ya maji yamepungua kwa mita 1,500 za mraba kwa hekta, na mapato kutoka hekta moja ya shamba yameongezeka kwa yuan 22,500.

    Habari zinasema, baadhi ya mikoa iliyoko magharibi mwa China itaendelea kueneza matumizi ya teknolojia hii, ili kuongeza ufanisi ya matumizi ya maji, na kuyasaidia maeneo yanayokumbwa na ukame kuongeza uzalishaji wa kilimo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako