• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawakili wa kesi ya Pistorius waanza kutoa maelezo ya mwisho

    (GMT+08:00) 2014-08-08 15:52:46

    Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanaridha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, umeanza kutoa maelezo ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo. Hii ni kabla ya mahakama kutoa hukumu ya mwanariadha huyo. Pistorius anatuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp, nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka jana. Wakili wa upande wa mashitaka Gerrie Nel amesema si sahihi kuwa Pistorius alimpiga risasi mpenzi wake kimakosa akidhani kwamba alikuwa jambazi. Mauaji hayo yalitokea tarehe 14 mwezi Februari mwaka jana. Wakili wa Pistorius pia anatarajiwa kutoa maelezo yake ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo. Hata hivyo wakili huyo wa upinzani ameiambia mahakama haipaswi kuwa na ugumu wowote katika kukataa ushahidi wa Pistorius kwa sababu hauna msingi na kwamba ni uongo. Pia amesema Pistorius amejidai kuwa ameathirika kwa njia moja au nyingine kutokana na ulemavu wake. Babake Pistorois ambaye hajawa maishani mwake kwa miaka mingi alikuwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo kuanza kusikilizwa. Babake marehemu Reeva pia alifika mahakamani kwa mara ya kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako