• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya pili ya Olimpiki ya vijana kufungwa kesho

    (GMT+08:00) 2014-08-27 17:34:51

    Michezo ya pili ya Olimpiki ya vijana ya majira ya joto itafungwa kesho mjini Nanjing, China. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atahudhuria sherehe ya ufungaji wa michezo hiyo, na mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya kimataifa Bw. Thomas Bach atatangaza kufungwa rasimi kwa kwa michezo hiyo. Michezo hiyo si kama tu imevutia wageni kuja China, bali pia imewapa fursa wageni kujionea historia ya China, na haswa historia ya mji wa Nanjing. Fadhili Mpunji anaeleza zaidi

    Mkuu wa Ujumbe wa Olimpiki wa Rwanda Elie Manirarora alisema, aliwaleta wachezaji kushiriki kwenye michezo hiyo, sio tu alitumaini kuwa wataweza kupata matokeo mazuri katika mashindano, muhimu zaidi ni kwamba vijana wao watajionea China na kuifahamu China wakati wa michezo hiyo. Bw. Elie alipendekeza wachezaji na wageni kutembelea jumba la makumbusho ya mauaji makubwa ya Nanjing ili kuifahamu historia hiyo. Bw. Elie alisema kama vijana hao wanaweza kujionea ukatili wa vita, watalinda zaidi amani iliyopo.

    "Michezo ya Olimpiki ya vijana ni fursa nzuri ya kufahamu historia na kutupia macho siku za baadaye. Mashindano si lengo la pekee la michezo hii, mbali na mashindano, naona muhimu zaidi ni mawasiliano. Naona ni afadhali kwa wageni kuja hapa kutembelea Jumba hili lenye umuhimu mkubwa wa kihistoria. Kama hatujionei kwa macho yetu wenyewe, hatutafahamu historia, na tutashindwa kutupia macho siku za baadaye. Kama wachezaji wetu, marafiki wenzetu wageni, na vijana wetu wakija kutembelea jumba hili, wataifahamu historia hiyo, watapenda zaidi amani na utulivu, na kuacha mauaji, kwa kuwa jambo hilo ni janga kubwa kwetu."

    Msichana Namrisha ni mwanafunzi kutoka Mauritius anayesoma nchini China. Alisema kila mara anapokwenda kutembelea jumba hilo, anapata ufahamu mpya.

    "kwa wageni, jumba hili linaweza kuwasaidia kuifahamu Nanjing, na mambo yaliyotokea hapa. Jumba hili linaweza kusaidia watu kufahamu historia ya hapa, naona kila mtu anapaswa kujua yaliyofanywa na Japan dhidi ya China. Inasikitsha kuona wachina walivyoteswa na kudharauliwa katika historia hiyo."

    Michezo ya Olimpiki ya vijana ya Nanjing si kama tu imeweka jukwaa la mashindano kwa vijana duniani, bali pia imetoa fursa kwa vijana kuifahamu Nanjing na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako