• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Madagascar wakutana

    (GMT+08:00) 2014-08-28 19:42:18

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amekutana na waziri mkuu wa Madagascar Bw. Kolo Roger ambaye yuko ziarani hapa China kuhudhuria sherehe ya kufungwa kwa Michezo ya pili ya Olimpiki ya Vijana.

    Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kushirikiana na Madagascar kuimarisha uaminifu, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika sekta za nishati, kilimo, mifugo na uvuvi, mafunzo ya nguvukazi na kupunguza umaskini, na kuinua uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya.

    Kwa upande wa Bw. Kolo Roger, amesema Madagascar inatarajia kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako