• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanne wafariki na wengine 32 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2014-08-28 20:55:06

    Watu wanne wamefariki na wengine 32 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo mjini Voi, kaunti ya Taita Taveta, nchini Kenya, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia.

    Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Richard Bitonga amesema, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, basi hilo lililokuwa likielekea mjini Mombasa kutoka Voi, halikugongana na gari lingine, bali dereva wa basi hilo alishindwa kulidhibiti na hivyo kuacha njia.

    Takwimu zilizotolewa na Wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya Kenya zinaonyesha kuwa, ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 50 tangu sheria mpya za barabarani zianze kutumika nchini humo mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako