• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yazindua mpango wa kukabiliana na Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-29 08:51:32
    Shirika la Afya Duniani WHO limezindua mpango wa kutoa mwongozo na kuratibu harakati za kimataifa za kupambana na mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi. WHO imesema, lengo la mpango huo ni kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Ebola duniani ndani ya miezi sita hadi tisa, ambapo asilimia 40 ya wagonjwa wa Ebola wamegundulika ndani ya wiki hii tatu. Kutokana na mpango huo kipaumbele kitawekwa katika mahitaji ya matibabu na vituo vya usimamizi, uhamasishaji, na kuhakikisha mazishi ya waliokufa kutokana na Ebola yanafanyika salama.

    Habari nyingine zinasema daktari mmoja wa Nigeria katika mji wa Port Harcout jana alithibitishwa kufariki, na kufanya idadi ya watu waliokufa kutokana na homa ya Ebola nchini Nigeria kufikia sita. Na serikali ya Marekani imetangaza kuwa wiki ijayo itaanza majaribio ya chanjo ya Ebola kwa binadamu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako