• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China awakaribisha wageni wa heshima waliohudhuria ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing

    (GMT+08:00) 2014-08-29 09:40:19

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa shukrani kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa na nchi mbalimbali duniani kutokana na uungaji mkono, mwitikio na usaidizi wao kwa Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing.

    Akihutubia hafla ya kuwakaribisha wageni waliohudhuria ufungaji wa Michezo ya pili ya Olimpiki ya Vijana ya majira ya joto uliofanyika jana mjini Nanjing, waziri mkuu Bw. Li Keqiang amesema wachezaji wa nchi na sehemu mbalimbali wamepata mafanikio makubwa viwanjani na kujionea tamaduni za aina mbalimbali nje ya viwanja, jambo ambalo limesukuma mbele maendeleo ya michezo ya Olimpiki, kuonesha moyo wa Olimpiki wa "umoja, urafiki na amani" na kujenga daraja la mawasiliano.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Bw. Thomas Bach, mwenyekiti wa heshima wa kamati hiyo Bw. Jacques Rogge, mawaziri wakuu wa Djibouti, Madagascar, Croatia pamoja na Antigua na Barbuda wamehudhuria hafla hiyo. Kabla ya hapo, waziri mkuu wa China Li Keqiang alifanya mazungumzo mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Bw. Thomas Bach.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako