• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini kufanya mageuzi ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2014-08-29 10:54:17

    Serikali ya Afrika kusini itaendelea kutekeleza sera ya fedha inayosaidia serikali kuokoa pesa wakati wa hali nzuri ya uchumi na kuzitumia kwa ajili ya kutuliza uchumi wakati wa hali mbaya.

    Naibu rais wa nchi hiyo Bw Cyril Ramaphosa ameeleza kuwa hili ni moja ya malengo ya serikali ya kufanya mageuzi ya uchumi kwa kiasi kikubwa ambayo yatakuwa na tofauti yenye ubora. Aidha amesema wanataka sera ambayo itahamisha hatua kwa hatua matumizi ya fedha na kupeleka kwenye uwekezaji. Bw Ramaphosa amesema serikali inaona kuna nafasi kubwa zaidi kwa mashirika ya kifedha katika kusaidia uwekezaji kwenye miundo mbinu, kilimo, maendeleo ya biashara ndogo ndogo, kuwawezesha waafrika kusini weusi kiuchumi na kuendeleza viwanda.

    Pia amefafanua kuwa benki zitahamasishwa kupanua huduma za upatikanaji wa fedha ili kuwawezesha watu kuendeleza raslimali zao na kusaidia biashara ndogo ndogo kukua zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako