• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaandaa kwa mafanikio michezo ya Olimpiki ya vijana

    (GMT+08:00) 2014-09-01 15:37:22

    Hujambo msikilizaji na karibu katika kipindi cha China Machoni Mwetu, mimi ni Fadhili Mpunji niko na mwenzangu Pili Mwinyi. Leo katika kipindi hiki tuna mada ya michezo. Tunajadili mada hii baada China kuandaa kwa mafanikio michezo ya Olimpiki ya vijana, iliyofanyika mjini Nanjing, mkoani Jiangsu. Michezo ambayo iliwashirikisha vijana kutoka katika nchi karibu zote duniani, ikiwa ni pamoja na vijana kutoa nchi za Afrika Mashariki.

    Pili: Wengi tumezoea kusikia michezo ya Olimpiki ambayo huwa inafanyika kila baada ya miaka minne, michezo ya Olimpiki ya wakubwa, na itakayofuata ni ile itakayofanyika kule Rio De Janeiro nchini Brazil. Lakini mwezi huu michezo ya Olimpiki ya vijana wa China imefanyika katika mji wa Nanjing hapa China na kuhudhuriwa na watu wengi. Kwa mara nyingine tena, michezo hii imeonesha ukarimu wa wachina na uhodari wao kwenye michezo.

    Fadhili: Lakini mbali na ukarimu wa wachina, wanamichezo walikuwa na matarajio mengi. Kwa mfano mwanariadha wa Kenya Gilbert Kwemoi mwenye umri wa miaka 17, alipata medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 1500 kwa wanaume. Hii ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye mashindano makubwa kama hayo. Mbali na kufurahia ushiriki wake anasema lengo lake kubwa ilikuwa ni kupata medali ya dhahabu.

    Pili: Kama tulivyomsikia Bw Kwemoi, lengo lake kubwa ilikuwa ni kupata medali ya dhahabu. Lakini lengo la maandalizi ya michezo ya pili ya olimpiki ya vijana, mbali na kutaka vijana washindane pia ilikuwa ni kufanya michezo hiyo iwe fursa muhimu kwa wanamichezo vijana kutoka sehemu mbalimbali na kuonesha maelewano na ushirikiano bila kujali wanatoka wapi na wanaonekana vipi. Mbali na mashindano yenyewe, michezo hiyo pia ni daraja la urafiki na maelewano kati ya wanamichezo vijana wa nchi mbalimbali. Shughuli mbalimbali za utamaduni na elimu pia zilifanyika kwenye kijiji cha michezo ya Olimpiki ya vijana.

    Fadhili: Tukiangalia lengo la michezo hii, tunaweza kujiuliza na kuanza kujiangalia sisi wenyewe. Hivi tunashiriki kwenye michezo na wengine, kwa lengo la kujenga urafiki au ni kwa lengo la kutafuta ushindi tu. Au kwenye jamii zetu tunaichukuliajie michezo? Ni kupoteza muda tu au ni burudani tu na kutafuta ushindi. Labda wewe pili ulipokuwa ukicheza michezo lengo, lengo hasa lilikuwa nini?

    Pili: Naibu katibu mkuu wa kamati ya olimpiki ya Kenya Bw. James Chacha anaona kuwa, tofauti na michezo ya Olimpiki ya wakubwa ambayo lengo kubwa ni ushindani, michezo kama Olimpiki ya vijana inapaswa kutumiwa katika kuondoa vikwazo vya kiutamaduni, na kuimarisha maelewano kati ya wanamichezo wanaotoka kwenye tamaduni tofauti.

    Fadhili: Hapa China hali ni tofauti sana na kwenye nchi zetu ambako naweza kusema shughuli za michezo ni za kawaida sana. Hapa China wenzetu huwa hawapati muda wa kucheza mara nyingi wao wanakuwa busy na kazi. Lakini wanapotata fursa ya kucheza, wanatumia fursa hiyo kufahamiana zaidi na hata kuongeza mawasiliano kati yao.

    Pili: Katika kijiji cha michezo ya Olimpiki ya vijana, shughuli mbalimbali za utamaduni zenye umaalum wa nchi mbalimbali zilifanyika. China ilijenga jumba la utamaduni wa China. Katika jumba hilo, wanamichezo wa nchi mbalimbali walisaidiwa na watu wanaojitolea kupiga ala za muziki wa jadi za China, kujifunza sanaa ya maandishi ya kichina na kujifunza maongezi ya kawaida ya kichina.

    Fadhili: Lakini hata huko nyuma wenzetu wa Nairobi walifanya mahojiano na baadhi ya wanamichezo ambao walikuwa wanajiandaa kuja China kwenye michezo hii, kitu ambacho walikuwa wanasema mbali na kushindana walikuwa na lengo la kujifunza mambo kadhaa kuhusu China na wachina. Mwezetu Hamis Darwesh aliongea na Edgar Hafuni ambaye alieleza jinsi walivyojiandaa.

    Pili: Msikikizaji huyo Edga Hafuni ameeleza kuwa mbali na michezo, alipenda kujifunza utamaduni na hata mambo yanayohusu nchi yake Kenya na China. Sina hakina kama vijana wengi wana moyo kama huo, lakini naona kama michezo ikiwa ni sehemu ambako vijana wanafundishwa hata kujua mambo ya uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mwenyeji na nchi wanakotoka washiriki, litakuwa ni jambo zuri sana.

    Fadhili: nadhani litakuwa jambo zuri kwa sababu huwa tunasikia wachezaji wanashiriki kwenye michezo lakini hatujui kama kuna lolote ambalo wanajifunza na kurudi nyumbani kuwafundisha wenzao waliobaki. Nilifurahi pia niliposikia mwenzetu Hamis Darwesh akiongea na Bi Winfrey Njubike kuhusu lengo lake kwenye mashindano haya ya olimpiki ya vijana. Lakini ajabu ni kuwa aliwahi kushiriki kwenye mashindano na wachina lakini bahati mbaya ni kuwa hajui lolote kuhusu wachina, hili kidogo naona ni jambo la ajabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako