• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muhila mpya wa masomo waanza huku mageuzi yakianza kutekelezwa

    (GMT+08:00) 2014-09-01 18:58:57

    Wanafunzi nchini China wameanza muhula mpya wa masomo hii leo, wazazi wakifurahia hatua mpya zilizochukuliwa zinazolenga kuinua hadhi ya elimu nchini.

    Kwa miaka kadhaa sasa, jamii ililaumu uandikishaji wa wanafunzi katika shule za msingi na za kati kuwa hazina usawa na uwazi. Ili kuhakikisha maisha mazuri ya baadaye kwa watoto wao, wazazi matajiri walifanya kila linalowezekana kuwaandikisha watoto wao katika shule bora zaidi. Kuanzia kutoa maelfu ya Yuan kwa ajili ya ada ya kuchagua shule, hadi kuwapatia zawadi kubwa maofisa wa shule hizo, ushindani katika uandikishaji wa wanafunzi ni mkubwa sana nchini China, ambako elimu ni moja ya vipaumbele kwa wazazi kwa ajili ya watoto wao. Lakini kwa mwaka huu, kanuni mpya za mageuzi zinazolenga kuleta usawa zimeanza kutekelezwa.

    Kutokana na serikali kuu kutaka usawa wa mgao wa rasilimali, imetunga kanuni mpya zitakazosaidia shule kukabiliana na vigezo vya juu na kuzuia ada kubwa za kuchagua shule, pia serikali kuu inatunga kanuni mpya zitakazowafanya wanafunzi kuchagua shule zilizo karibu na makazi yao.

    Wazazi, wakiwemo vibarua kutoka vijijini katika mji wa Beijing, mashariki mwa mkoa wa Shandong nchini China, na mkoa wa kaskazini wa Hebei, ambako mageuzi yameanza kutekelezwa mwaka huu, wamesema hakuna ada yoyote iau zawadi (rushwa) ziliyzotakiwa wakati wa kuwaandikisha watoto katika shule zenye ubora wa juu, ali mradi tu wanaishi kwenye eneo karibu na shule hizo.

    Wakati huo huo, shule zenye ubora wa juu nazo zimeagizwa kuinua ubora wa elimu kwa kuchangia rasilimali za kufundishia na kuzisaidia shule zilizo nyuma kuboresha elimu kwa kupeleka wasimamizi wakufunzi katika shule zisizo na ubora unaotakiwahizo. Katika hatua nyingine, shule zenye ubora wa juu huungana ili kutumia vizuri rasilimali hizo.

    Hata hivyo, familia tajiri bado zinatafuta njia ya kuzunguka utaratibu huo. katika kesi nyingine, wazazi hao wanaweza hata kununua nyumba katika wilaya ambazo shule hizo zipo. Wakala wengi wa nyumba wamepata faida kutokana na manunuzi ya nyumba hizo, ambazo zinauzwa kwa bei kubwa zaidi hususa zile zilizo karibu na shule nzuri.

    Wataalam wanapendekeza mabadiliko ya taratibu na ya ufanisi katika kugawanya shule ili kuhakikisha kila wilaya ina shule bora moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako