• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya kimataifa ya Wu shu yafanyika Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2014-09-01 19:33:04

    Mashindano ya kimataifa ya michezo ya WUSHU yalifanyika wikiendi iliyopita katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Michezo hiyo inazikutanisha timu zipatazo 20 kutoka mikoani mbalimbali ya Tanzania, na kutoka nchi jirani ikiwa ni pamoja Zambia, Uganda na Zimbabwe. Walimu na waamuzi wa mchezo wa Wu Shu kutoka China pia wanashiriki kwenye michezo hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuleta uhalisia wa michezo hiyo.

    Lengo la mashindano hayo ni kuwahamisha vijana wa watanzania na wengine kutoka nchi karibu na Tanzania, kushiriki kwenye michezo ya kung fu. Haya ni mashindano ya pili kufanyika nchini Tanzania na safari hii yameonesha kuvutia watu wengi zaidi kuliko yale ya awali. Mbali na kuvutia wanamichezo na wapenzi wengi wa mchezo wa wu shu, safari hii makampuni mengi pia yameonesha mwitikio mzuri wa kuunga mkono michezo hiyo. Mbali na makampuni ya wafanyabiashara wa China walioko Tanzania, makampuni ya wenyeji pia yamejitokeza kuunga mkono mashindano hayo.

    Hata hivyo baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wanaona kuwa mwitio ulikuwa mkubwa kuliko matarajio, na kufanya mazingira ya mashindano yawe na msongamano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako