• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya China, Ulaya na Asia yafanyika mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2014-09-01 19:47:15

    Maonesho ya nne ya China, Ulaya na Asia yatakayofanyika kwa siku sita yamefunguliwa huko Urumuqi mkoani Xinjiang, China.

    Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni "kufungua na kushirikiana kwa ajili ya kujenga eneo la kiuchumi la njia ya hariri", ambayo yanalenga kuvutia jumuiya za kiuchumi za kikanda kujadili mkakati wa maendeleo.

    Pendekezo la Eneo la kiuchumi la Njia ya Hariri lililotolewa rais Xi Jinping wa China wakati wa ziara yake katika nchi za Asia ya Kati mwezi Septemba mwaka jana, limetia nguvu katika ushirikiano wa kikanda wa Ulaya na Asia.

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Wang Yang amehudhuria ufunguzi wa maonesho hayo pamoja na waziri mkuu wa Kazakhistan, waziri mkuu wa Kyrgystan, na naibu spika wa bunge la Georgia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako