• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia zaanza ujenzi wa bomba la gesi kati yao

    (GMT+08:00) 2014-09-02 09:40:13

    Naibu waziri mkuu wa China Zhang Gaoli ambaye yuko ziarani nchini Russia na rais Vladimir Putin wa Russia wameshiriki kwenye sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa bomba la gesi katika njia ya mashariki zilizofanyika mjini Yakutsk, Russia.

    Akizungumza na rais Putin, Bw. Zhang amesema ujenzi na uendeshaji wa bomba hilo vitatoa nishati salama na safi inayotegemeka kwa maendeleo ya uchumi wa China na pia kutoa soko tulivu la muda mrefu kwa Russia yenye utajiri mkubwa wa maliasili ya gesi. Ameongeza kuwa bomba hilo pia ni muhimu katika kuingiza uhai kwa maeneo ya viwanda ya jadi kaskazini mashariki mwa China na maendeleo ya Mashariki ya Mbali ya Russia.

    Kwa upande wake rais Putin ameshukuru msukumo mkubwa uliofanywa na mwenzake wa China Bw. Xi Jinping kwa ushirikiano wa gesi kati ya nchi mbili, na kuwa na matarajio na mazungumzo watakayofanya katika siku chache zijazo. Amesema hivi sasa ushirikiano kati ya Russia na China uko katika kiwango cha juu, na Russia inapenda kuimarisha ushirikiano huo katika sekta ya nishati na maeneo mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako