• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yatangaza hatua mpya za kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2014-09-02 11:02:22
    Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema, nchi hiyo itachukua hatua kali zaidi za kupambana na ugaidi.Hatua zilizotangazwa ni pamoja na kutunga sheria ya kuwapa polisi madaraka ya kushikilia paspoti za watuhumiwa wa ugaidi kwenye mipaka ya Uingereza; kuwazuia magaidi ambao ni raia wa Uingereza kuingia nchini humo, na kuzitaka kampuni za ndege kutoa taarifa juu ya safari za abiria kwenye maeneo yenye migogoro.Ijumaa iliyopita serikali ya Uingereza ilitangaza kuongeza kiwango cha tishio la kigaidi nchini Uingereza kuwa cha juu zaidi, ikiwa na maana kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa nchi hiyo kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako