Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki-moon ameeleza kushtushwa na Israel jana kutangaza kuwa eneo la Bethlehem kwenye ukingo wa magharibi lenye hekta 400 ni sehemu ya taifa lake. Amesema kujitwalia eneo kubwa la ardhi kama hilo kunaweza kuifanya Israel kujenga makazi mengi zaidi, jambo ambalo ni haramu chini ya sheria ya kimataifa na kwenda kinyume na juhudi za kutafuta suluhisho la kuwepo kwa nchi mbili za Palestina na Israel.
Bw. Ban pia ameitaka Israel kutii wito wa jumuiya ya kimataifa wa kuacha shughuli za kujenga makazi na kufuata ahadi yake chini ya sheria ya kimataifa. Serikali ya Israel imesema eneo hilo halijatangazwa kumilikiwa na wapalestina, na kuongeza kuwa kuna kipindi cha siku 45 cha kufungua pingamizi dhidi ya uamuzi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |